macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 25,191
- 48,765
Natafuta wachezaji kutoka afrika hasa watanzania kuja kujaribu soka hapa.
Uwezekano wa kupata timu ni mkubwa kama yeye ni mchezaji maana atajaribiwa ktk timu nyingi na za daraja tofauti.
Asiwe na umri unaozidi miaka 23.
Awe na uwezo wa kujigharamia Ticket
Maradhi na chakula akiwa hapa yatafanywa na kampuni.Mwariko atatumiwa na kampuni wa kuja kujaribu soka hapa
Kwa vile tz haiifahamiki kisoka tutahitaji wachezaji wa mwanzo wawe wanasakata kabumbu kisawasawa ili wapeperushe jina .
pia unaweza tembelea ktk web yetu .
www.nowakconsulting.pl
Nitwangie sms +48697461457 andika jina lako na klabu unayocheza mimi nitakutwangia simu moja kwa moja.
Ama nitwangie Email mkamap@yahoo.com ama uni PM ukibainisha namba yako ya simu.
ustaraabu Nimatumaini yangu hatuta ABUSE mawasiiano .Na ni mategeo yangu ujumbe tutawafikishia wahusika .
Otherwise ON PEACE !!!! C U then.
Ni kweli kabisa na wewe ni mmoja wa mifano hai, ni wazi umekurupuka kuweka hili tangazo hapa, hukufikiri. Kuna issues nyingi ambazo ungeweza kuzifine tune kabla ya kuanza kuutangazia ulimwengu kile unachotaka kufanya.
Huo utapeli wako unaotaka kutumia umepitwa na wakati!!! Wachezaji wanatafutiwa kwenye internet au viwanjani? Kama huna uwezo wa kusafiri kwenda kuchagua... huo uwezo wa kuwalisha na kuwalaza utaupata wapi?
Mkamap,
Mkuu nakuomba sana uyasome maelezo ya jamaa waliotangulia na kuyapa umuhimu achana na hizo lugha walizotumia, lakini chukua points nzingi nzuri ambazo zitakusaidia na pengine kukuepusha na Balaa.
Majuzi nilikuwa nikiangalia kipindi kimoja cha BBC kuhusu Ma Agent wa Soccer nchini France jinsi walivyoharibu biashara hiyo kwa kuwavuta vijana wadogo sana toka Afrika Magharibi wakiwaahidi kuchezea timu za France. Lakini baada ya hao vijana kutopata usijiri ktk timu hawa Maagent waliingia kizani hivyo kuwabidi vijana hao kuwa Machinga wa Ulaya. Sasa basi serikali ya France imeanza kupeleleza kuhusiana na Maagent hao jinsi wanavyofanya kazi na ikiwezekana kuwafungulia mashtaka..
Kwa hiyo mkuu nadhani hoja kubwa hapa ni ushauri wa watu ujipange kisawasawa kwanza, kusajiri kampuni mtu yeyote anaweza kufanya hivyo nchi za Ulaya hakuna taabu kama nyumbani isipokuwa tu kile kityakacho fuatia ndio kinaweza kukuharibia maisha kabisa.
Binafsi, ningekushauri mbali na kusajili Ulaya sajili pia Bongo ambako utamweka mtu maalum kuchagua, kuvutia, na pengine visa za kusafiria kwa wale waliobahatika...
Mtego mkubwa hapa ni visa zaidi ya tiketi, kwa sababu wapo watu kibao Bongo wanaweza ku raise hizo 1.3 millioni kwa ajili ya tiketi isipokuwa hukwama kwenye visa. Hivyo basi, isiwe swala la kuvuta tuuu watu Ulaya kubmuka hii ni biashara huhitaji kucheza kamali wala kuogopa maji kuyakoga..
Unahitajika ku invest ktk vijana hao na mara nyingi navyofahamu Hata akitoka timu kubwa za gdaraja la kwanza watahitaji uwalipe fedha wao kama timu iliyomsajili, huyo kijana atazipata wapi?...Hivyo akiwa ktk mtihani huko Ulaya ni lazima uwe na makubaliano na timu iliyomsajili laa sivyo unatafuta vijana wasioweza kuucheza na sidhani kama Ulaya watapata nafasi ya kujaribu mtu ambaye hata kwetu Afrika hajawahi kuchezea daraja la kwanza.
Ndio hayo tu mkuu, huu ni ushauri unaweza kuuweka kando ukaendelea kubangaiza...Lakini kwa jinsi navyofahamu Ma agent wanavyofanya kazi mkuu hata kupata toka Nigeria na sijui wapi itakuwa ngumu..
Hii ni news nzuri sana,Shukurani kubwa kama utaweza kusaidia vijana wetu...Hongera Sana
Hio lugha ya kipolish na bongo wapi na wapi?
Web site----Polish
Simu-----Sweden....mhmhmhmh!!!!!!!!!
Mkuu, mkamap.
Mimi nafikiri wazo lako si baya na ni muhimu kuzingatia lengo lako la kuinua vipaji vya soka vya vijana wa kitanzania.
Lakini mimi nakuuliza swali la msingi kabisa, je umewasiliana na TFF, BMT na vilabu vya soka vya Tanzania?
Pili je umefanya utafiti upi mpaka ukaona kwamba unaweza kuinua vipaji vya soka vya hao vijana unaowahitaji hasa katika soka la Ulaya?
Maswali haya yanaenda na mifano ya vilabu vya soka vya Nigeria, Ghana na Ivory Coast ambao wana mikataba na ushirikiano na FAs na vilabu vya soka vya Ulaya ambapo kunatengenezwa Avenues za vijana kwenda kufanya majaribio ya wiki mbili tau na sio miaka.
Sasa naomba pia utoe potfolio yako au profile ili tukufahamu na labda tuweze kukuchangia katika jitihada zako za kukuza soka la Tanzania.
Mwisho waambie hao wa-Poland waweke pia lugha ya kiingereza kwenye tovuti yao maana wengine hatujui ki-"polish".
Shukran.
www.nowakconsulting.pl
akiwaza nitampa mkataba ausasambue kama atakavyo
Otherwise Atakua mvivu wa kufikiri na ukurupukaji usio na msingi.
Mkuu nashukuru kwa maswali yako
Mkuu mimi sijasema ninamikakati ya kuinua viwango vyao .Ila kampuni inahitaji wachezaji kutoka afrika na mimi kama mbongo nikaitia ushawishi tuchukue wabongo lengo ni kua wakipata timu lengo la kwanza mifuko yao itatuna wenda wakaongeza bangaloo pale mwembeyanga ,pili kiwango kitakua chenyewe kama wanabidii na hatimaye kiwango cha STARS.
Kampuni ina timu ambazo zipo tayari kuwajaribu daraja la kwanza ,lapili maana saizi ndio muda muafaka wa usajili.
Mchezaji akija akifika anapumzika siku mbili siku mbili anajaribiwa anaenda klabu ya pili na ya tatu naya mwisho.Anasaini mkataba na timu ama tunamsindikiza uwanja wa ndege .
Tumeelewana mkuu ama bado
Sasa basi waunganishe na TFF maana kama nimekuelewa wewe unakuwa kiunganishi hapo.
Ila wenzako woote huenda Africa au field yoyote ile na unapo-spot talents zozote zile unaandaa taratibu za kuhamishia hizi talents huko Poland.
Sasa kuna masuala ya UHAMIAJI, International Clearance na mengine. Kwa hio ujue hapa usiishie tu kujitangaza hapa bali hata katika magazeti ya nyumbani Tanzania si unazo fwedha kaka?
Pia hapa ndio swali langu la msingi linaingia kutaka kujua je wewe una sifa gani za kuwa "agent" au "middleman" katika hii kampuni?
Ila wazo lako ni zuri na nakutakia mafanikio mema.
tatizo letu sisi wabongo kila mmoja amegeuka kua mwanasiasa mimi nimeomba contact za wachezaji lakini mtu anajitahidi kuligeuza kua siasa.
Usizungumzie kabisa masuala ya uvivu hapa kwa kuwa wewe ndio kinara, kwanini utudirect kwenye website ya kipolish? watanzania wangapi wanajua hiyo lugha? Kama hiyo agency yako imeamua kufanya scouting world wide kwanini wasi update hiyo website yao na kuiweka katika lugha za kimataifa? Na kwanini haupo tayari kusafiri kwenda bongo kuidentify vijana wenye vipaji kabla hawajachoma nauli zao kuja huko wakati hakuna guarantee kwamba watasajiliwa?Unajua thamani ya Tshs 1.3m kwa mtu anayetoka familia ya kimaskini? Ni wazi kwamba agency yako ina uwezo mdogo kifedha, achilia mbali kutoweza kuwalipia nauli vijana wenye vipaji kuja huko kwa majiribio, inaonekana hata kujilipia nauli ya kwenda bongo kufanya scouting ni mgogoro kwenu.
Mimi ninachoweza kusema ni kua Hakuna docomenti ya kiingereza,kiswahili ,kijerumani,kichina,kijapani ama lugha yoyote tofauti na polish inayowezwa sainiwa na mahakama nchini hapa.
wala hakuna mwanasheria hapa anaye process dokomenti za lugha za kimataifa yani kiingereza ,kifaransa na kispanish na zinginezo tofauti na polish.
Usije tu ukasema hakuna website inayoruhusiwa kuwa katika lugha nyingine zaidi ya kipolish hapo!
sawa sawa mkubwa wewe mtaaalamu tunakuamini endelea na juhudi hizo hizo na ubarikiwe sana .
Mkamap,
Dont get me wrong bro, labda una nia njema kabisa lakini my problem ni jinsi ambavyo umeipresent idea nzima, hili ni suala zito so I would advise you to take your time, do some research halafu urudi na kitu kamili ambacho kitakuwa crystal clear kuepuka maswali mengi.