Sikuifanya mkuu, niliajiri vijana ambao wapo shamba wanakaa huko huko nawalipa kwa mwezi, wao ndio walitoa hivyo visiki na kazi zingine zote za pale wanazifanya, mimi na wao malipo ni mwisho wa mwezi.
Nilifikiria kung'oa tu visiki nilipe watu kisha waondoke, ije kazi nyingine nilipe watu tena kisha waondoke nikaona ni uchezeaji pesa kwakuwa malengo ya mbele nayajua basi ikabidi niajiri vijana, nimefanikiwa pata wawili.
Hapa natafuta wa mwisho mmoja waungane wawe watatu kisha rasmi nikianza project zangu najua nina majembe yangu matatu.