Wasiliana na Mstimbe Spiderman wa TBC kuna jamaa walikuja TBC kwenye Kipindi cha Amka na Badilika kuna Mkenya Mmoja alichambua kuhusu ujenzi na ushauri na ufuatiliji kitaalam hadi raha.
Yule Mtaalam alisoma Marekani kama sikosei,na pia anamiliki mashamba hayo pia.
Watengenzaji wengi wa Bongo wasanii na sio washauri wazuri,maana wanatumia uzoefu na sio utaalam wa hali ya Sasa.
Huwa nafuatili sana Kipindi cha Amka na badilika,hata leo mchana nimeona marejeo yake lakini number zao sina.
Maana watalaam wote wa masuala ya Biashara wanaohojiwa na AMKA NA BADILIKA wao huwa hawana noma,wanakuunganisha na mhusika moja kwa moja.
Tafuta number ya TBC waombe number ya Mtsimbe au Spiderman wa kipindi cha Amka na Badilika.
Halafu yeye atakuunganisha na wajenzi hao wa Kenya ambao kwa muono wangu na nilipofuatilia kipindi chao siku ile anamuhoji ni kwamba Wamejipanga sana na hakuna longolongo kama hawa wa kibongo.