Wazee nimerambazarambaza sana nikitafuta webdesign software lakini naona kizungumkuti tu, hujui ipi ni ipi. Naombeni ushauri ipi bomba iliyopo kwenye market today ....Nataka ambayo itakuwa na vikorombwezo vya kila aina.
haya napokea ushauri.....moja...mbili.....tatu....anza.
Dizaidi f'lani unaonekana una roho korosho.Habari zako
hujasema kama wewe ni mwanafunzi unataka kujifunza au ni mtumiaji unataka updates kutoka kwa wenzako kama ni mtumiaji huwa unatumia aina gani au tu ni kazi ya ofc badala ya kupeleka kwa wataalamu umeona ufanye mwenyewe tu kwa kutumia software fulani fulani kwa sababu umesikia ni rahisi kutoka kwa washauri wako yote hii hujasema
Hata hivyo siku hizi kuna kitu kinaitwa cms content management system kuna tovuti nyingi zenye kutoa huduma ya tovuti yenye huduma hiyo kwahiyo ukinunua hiyo unachotakiwa ni kusema tu tovuti yako inahusu nini kama ni shule basi utapewa cms maalumu kwa ajili ya shule kama ni kuuza basi utapewa inayofanana na wewe kazi yako wewe itakuwa ni kutoa na kuweka vitu tu update zitafanywa na yule mtu aliyekupa cms kutokana na mkataba wenu
unaona maisha yalivyomarahisi ?
kwahiyo wewe kama sio mtaalamu au hujui mambo ya tovuti nakushauri ufanyie bidii zaidi fani yako uliyonayo halafu mambo ya tovuti tafuta watu waliosomea fani hii wanaoijua na wanaoifanyia kazi siku zote kwao utapata mambo mengi zaidi kwa sababu sio kazi zao
wewe endelea na uhasibu tu au uhandisi tu
Mkuu Mwazange,
Ungekuwa specific sana kuhusu aina ya tovuti unayotaka kuitengeneza, kama ni ya kibiashara, ni ya kifamilia, ni ya mambo yako binafsi n.k., ili tujue ni software gani itakufaa kwa kazi hiyo. Kwa namna ulivyoweka maelezo yako, mimi binafsi nashindwa kuelewa "Vikorombwezo" unavyotaka. Vikorombwezo ndivyo hasa vinavyoamua aina ya software utakayotakiwa kutumia ili kufikia lengo lako la kuwa na tovuti unayotaka. Kwa mfano iwapo unataka tovuti yako iwe na 'animations', lazima utumie softwares zenye uwezo huo, kama vile 'adobe dreamweaver', Flash, n.k. Na kama hutaki makorokoro mengi zaidi, basi zipo nyingine kibao sana ikiwemo MS Front Page, webpage-maker, Java DK n.k, ushindwe wewe tu.
Nadhani tupo pamoja!
Hapana watu wanatafuta ajira na kutafuta kazi kwahiyo awape kazi hiyo inayowahusu tusitake kufogr vitu halafu fani nzima ya ict isiheshimike