Natahadharisha mapema kama Wewe ni Mwanayanga na una matatizo ya Moyo / Presha Kesho tulia Nyumbani Uugulie vizuri Kipigo!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Wana Simba SC ' Kazi Imekwisha ' na popote pale ulipo anza Kusheherekea kwani tunashinda Goli 2 kwa 0. Nitoe pia ONYO mapema kwa wana Yanga SC kama unajijua kabisa una matatizo ya Moyo / Presha na huwezi ' Kuvumilia ' tafadhali Kesho baki tu Nyumbani Kwako ukisikilizie vizuri ' Kipigo ' ukiwa Kitandani au Sebuleni Kwako kutokea Uwanja wa Taifa.

Na kwa Wanasimba hakikisheni mmeshakata ' Tiketi ' zenu zote na mkaujaze Uwanja kwani moja ya ' Sharti ' tulilopewa ' sehemu sehemu ' ni kwamba ili ' Majini ' yetu yafanye Kazi ya ' Kutukuka ' pale Uwanjani Taifa yanahitaji kuona rangi nyingi za Nyekundu na Nyeupe kwani kwa Kesho tutatumia sana Njiwa Watatu ila Njiwa mmoja ' atakufa ' pale pale Uwanjani na watabaki hao Njiwa Wawili ila kuna Paka Wawili Weusi mtawaona hasa Jukwaa linalotazamana na Chuo Kikuu cha DUCE wanapitapita hivyo msiwadhuru wala kuwafukuza hata kama wakiamua kuja Kukaa / Kuketi nanyi katika Viti vyenu.

Msipojaza Uwanja mpaka pomoni / juu ya uwezo basi SImba SC Kesho tunafungwa hivyo mkiona Kesho tumefungwa na Yanga SC basi msimlaumu yoyote yule bali mjilaumu nyie Wenyewe kwa kushindwa Kujitokeza kwa wingi na Kuujaza Uwanja. Kakateni ' Tiketi ' zenu upesi ili Watu wa Yanga SC wasizipate na wasiangalie hiyo mechi ' Mubashara ' na Uwanja mzima tuujaze Sisi.

Mwisho kuna uwezekano mkubwa pia Mchezaji wetu mmoja ' Kipenzi ' kabisa ama akaumia vibaya au akaonyeshwa Kadi Nyekundu hivyo msiwaze wala kuwa na wasiwasi kwani hilo nalo ni moja ya ' Agano ' letu la ' Ushindi ' tuliloliingia kutoka huko ' sehemu sehemu ' kwa Yule Mama mwenye Ziwa moja huku Zanzibar.

Anzeni Kufurahi wana Simba SC kwani ' Kazi Imekwisha ' rasmi na Kesho Yanga SC anafungwa Goli / Bao 2 kwa 0 Taifa.

Nawasilisha.
 
Hahaaaaaaa haaaaa ha ha ha haaaaaaaaaaaaaa...yani nacheka kama SOLO nusu roboti....Mtoa post unajua kujipa moyo aisee dah...Nyie mnajiita sijui simba sijui paka HAMNA PA KUTOKEA iyo kesho..NARUDIA TENA, kichapo kipo pale pale kinawahusu Mikia Fc.
 
Ndiyo Manara mwenyewe Huyo, au hujui mkuu.

Nadhani hapa JamiiForums nimebakisha kufananishwa na Vladmir Putin au Donald Trump tu pekee. Na bahati nzuri kuna Members baadhi humu ( tena wenye Heshima zao na mmoja wao ni Mhadhiri wangu Mpendwa kabisa wa Chuo Kikuu ) wanamjua GENTAMYCINE ' kindakindaki ' wakiona hii ' post ' yako hawatachelewa Kuniunga mkono kwamba ' You're a CERTIFIED IDIOT kabisa.
 
Vipi Mkuu,zile maiti mbili kutoka kwenye ajali ya Kivuko Ukara Mganga alizowaagiza mlizipata?
 
PENGINE ULIWAHI KUTABIRI IKATOKEA LAKINI HIZI MECHI ZINAZOENDELEA USHAURI TU

NENDA UWANJAN AMA KULA KATV KAKO KIMYA KIMYA

NIKISOMA ULICHOPOST TOKA MAJUZI NAOGOPA KUFUNGUA HATA POST YAKO NAHISI... BALAA LINGINE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…