Nawashukuru wana JF ambao mmekuwa mstari wa mbele kumshauri huyu mdau. Ndg yangu Black African ushauri umepewa. Kimsingi mtaji ulionao unatosha kuanzisha biashara ya kiwango cha fedha hiyo 100,000/=. Pia soko kwa ajili ya biashara unayotakiwa kuanzisha liko ama katika eneo unaloishi au unakosomea kwani wadau wake ndo wanaotakiwa kuwa wateja wako. Mimi ninakupa ushauri huu:-
1. Nunua mifuko ya maji/barafu pakiti moja Sh. 1,000/= ambayo ina pcs 100 anafunga maji na kuyapoza kidogo kwenye fridge kisha kuyauza @ mfuko Sh. 50/=. Hapa una uhakika ya kupata gross income ya Sh. 5,000/= . Kazi ya kufunga maji ni nyepesi, haitumii muda mwingi na unaweza kuifanya kulingana na muda wako hata kama ni usiku, kama nyumbani kuna friji unaweka maji yako huko au ukatumia deli. Biashara hii unaweza kuwa unamwachia mtu ama mwenye duka au genge kwa makubaliano ua kumpa Commission. Itakulipa ndg yangu kwa ushauri zaidi tuwasiliane
2. Anzisha genge dogo kulingana na fedha uliyonayo. Biashara hii inahitaji uwe na msaidizi wakati unapokuwa shuleni au unapokuwa umetingwa na masomo. Pale unapokuwa na muda nawe simamia uongeze nguvu. Chagua vitu vidogo vidogo vinavyotumika sana kila siku majumbani mfano mkaa, vitunguu, mafuta ya kupima, pipi, n.k. Hapa unaweza kuuza vocha pia.
3. Fanye biashara ya kuuza vocha kwani zinabebeka na unaweza kuifanyia popote. Muhimu ni wateja wako kufahamu kwamba wewe ni muuza vocha.
Biashara hizi zote ukipata watu wa kushirikiana nao katika kununua mzigo itakupunguzia gharama mbalimbali na kuokoa muda wako. Pia kama unaweza kupata wateja maalum wa kuwauzia bidhaa hizi na nyinginezo kutaokoa muda wako na itakusaidia kukokotoa faida kwa wepesi ikiwa ni pamoja na kujifunza juu ya ukuaji wa biashara ya soko lako.
Mi niishie hapo. Ila nawaomba wana JF wengine muendelee kumpa ushauri huyu mwenzetu. Asante sana