Nataka hawa ndiyo wawe katika Benchi la Ufundi la Taifa Stars na siyo 'Goigoi' walioko sasa

Nataka hawa ndiyo wawe katika Benchi la Ufundi la Taifa Stars na siyo 'Goigoi' walioko sasa

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
1. Mecky Mexime Kocha Msaidizi

2. Ally Mayai Meneja wa Timu

3. Juma Kaseja Kocha wa Makipa

Kocha Mkuu Kim Poulsen hatufai ila awe Mkurugenzi wa Ufundi wa Timu za Taifa na atafutwe Kocha mwenye Viwango wa Kimataifa na anayejua Kucheza Soka la Kimalengo na siyo Soka la Hamasa, Siasa na Upuuzi.

Maoni yangu yaheshimiwe tafadhalini.
 
1. Mecky Mexime Kocha Msaidizi

2. Ally Mayai Meneja wa Timu...
Wala hiyo sio dawa, hata ulete benchi la ufundi la makocha wote wa ulaya, hatutoboiii!!tatizo letu hakuna wachezaji wenye kiwango cha kimataifa, mchezaji kwenye club yake ya ndani tu hapa anachoma mahindi, huyo ndiye uje kumtegemea kwenye timu ya taifa??

Wekeni mipango mikakati labda ya kushiriki kwanza kombe la Afrika mala nyingi halafu target iwe kushiriki sasa kombe la dunia la 2030!!sasa nyie inabakia wiki moja ndio mnakuja na HAMASA!!

Mkidhania kuwa kwenye mpira ni hamasa!!ligi yenyewe iko wapi ya kuwatengeneza wachezaji wako??angalia DRC, hakuna mchezaji hata mmoja wa tp mazembe, wala AS vital, ambao hapa Afrika ndio miongoni mwa timu bora, ambaye jana alicheza!!walishusha midude tu kutoka mbinguni huko, na mingine ilikuwa bench tu!!!
 
Kocha anayejua kucheza kimalengo alikuwepo Amunike, ila wabongo tulimsagia kunguni kisa hatuchezi soka lenye udambwi udambwi.

Kim huyu hapa, kaifanya Bongo kugeuka academy ya Barcelona. Sio kwa mipasi ile sio kwa visigino hivyo ila wachezaji wanamuangusha. Hata mpira wa kutap in tu mchezaji anabutua.
 
Waziri mkuu Leo amesema kina KARIA wajitafakali ,maana walijipitisha bila kupingwa.
 
Nasubiri Kesho ( Jumamosi ) kuna Kongamano la Wanawake ( akina Mama ) najua kama Kawaida yangu sitokosa wale walioishiwa Nauli kwa Sadaka ya Kujimaliza ili nikawabandue vizuri na Bwerere tu.
🤣🤣🤣🤣🤣Sadaka ya kujimaliza ndo ipoje
 
Nasubiri Kesho ( Jumamosi ) kuna Kongamano la Wanawake ( akina Mama ) najua kama Kawaida yangu sitokosa wale walioishiwa Nauli kwa Sadaka ya Kujimaliza ili nikawabandue vizuri na Bwerere tu.
🤣🤣🤣🤣🤣Sadaka ya kujimaliza ndo ipoje
 
1. Mecky Mexime Kocha Msaidizi

2. Ally Mayai Meneja wa Timu

3. Juma Kaseja Kocha wa Makipa

Kocha Mkuu Kim Poulsen hatufai ila awe Mkurugenzi wa Ufundi wa Timu za Taifa na atafutwe Kocha mwenye Viwango wa Kimataifa na anayejua Kucheza Soka la Kimalengo na siyo Soka la Hamasa, Siasa na Upuuzi.

Maoni yangu yaheshimiwe tafadhalini.
Ishu ni kwamba Watz hatujajaliwa kujua mpira, tubaki na mentality hiyo cku zote za maisha yetu kwamba ktk vitu ambavyo Watz hatujabalikiwa basi ni kutojua kucheza mpira, lkn pia co mpira tu bali ni michezo kwa ujumla.

Tuna kila kitu, tuna amani, viwanja vizuri ukilinganisha na viwanja vya vinchi vinavyotufunga kila siku hapa Afrika, wachezaji wa timu ya taifa wengi wao wanaishi vizuri, lkn mpira ndio hawajui, yn hawafundishiki.

Hizi Simba na Yanga tunazoziona angalau zinacheza vzr miaka ya karibuni ni kutokana na kusajili wachezaji wa kigeni, ukitaka kuamini jaribu kufuatilia cku simba na Yanga wakicheza wazawa wengi huwa ni mpira wa hovyo na wa papara usio na malengo, mfano jana mechi ya Yanga na kmkm kocha aliamua kuwaweka Watz wengi ambao wanakaa benchi tukaona jinsi walivyo hovyo, lkn Yanga hiyo hiyo ndiyo inayosifika kwa soka maridadi kwa ss but ukweli ni kwamba wanacheza vzr kwasababu asilimia kubwa ya wanaoanza kikosini co wazawa, huo ndio ukweli, sisi ni kichwa cha mwendawazimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kim poulsen anahusikaje na ubabaishaji wetu wa kufanya mambo kwa hamasa na zimamoto.Tatizo ni sisi wenyewe na siasa zetu ndo sababu hakuna mchezo wowote tunafanya vizuri.Kocha hana shida kwasababu anafubdisha wachezaji wa daraja la kati.
 
1. Mecky Mexime Kocha Msaidizi

2. Ally Mayai Meneja wa Timu

3. Juma Kaseja Kocha wa Makipa

Kocha Mkuu Kim Poulsen hatufai ila awe Mkurugenzi wa Ufundi wa Timu za Taifa na atafutwe Kocha mwenye Viwango wa Kimataifa na anayejua Kucheza Soka la Kimalengo na siyo Soka la Hamasa, Siasa na Upuuzi.

Maoni yangu yaheshimiwe tafadhalini.
sijui WASHAURI huwa wao wanashauriwa na nani.
 
Back
Top Bottom