Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tatizo unang'atwa na hofu. Angalia kama mapato ya biashara yako in terms of net profit kwa mwezi ni zaidi net salary yako. kwa mwezi. Cha pili angalia opportunity cost. Uko huru zaidi upande gani. Pia angalia uendelevu wa biashara yako kwa miaka 5 ijayo kama itakuwepo. Angalia una ujuzi gani na hiyo biashara pamoja na washindani wako ktk soko. Last but not least angalia uthubutu wako katika kujiajiri-entrepreneural ability. Hii ni rasilimali muhimu sana. Baada ya hapo kata shauri
Nashukuru kwa mawazo yote mazuri,
nimepaata idea mpya kwamba labda nichukue likizo isiyo na malipo kwa miezi mitatu plus annual leave nisome ramani na kuondoa hofu,kikieleweka basi niachie ngazi,
mnasemaje?
Wasiwasi ni akili mpendwa.
Ni vema ukaangalia faida unazopata kibaruani kwako na biashara pia. Uhakika ni muhimu juu ya mwendelezo wa biashara yenyewe isije kuwa ni ya msimu tu.
Endelea kutumia kazi kama dhamana kama haikubani sana katika shughuli zako binafsi. Ukipata faida kotekote huoni kuwa inalipa zaidi?
Haupo tayari, endelea na kibarua chako hapo NGO mkuu usitafute presha bure. In short you are not a 'business-type' guy, you are a 'salary-type' guy
Nashukuru kwa mawazo yote mazuri,
nimepaata idea mpya kwamba labda nichukue likizo isiyo na malipo kwa miezi mitatu plus annual leave nisome ramani na kuondoa hofu,kikieleweka basi niachie ngazi,
mnasemaje?
Kuna Professor wangu mmoja amenifundisha enterpreneurship and Innovation alituambia darasani hivi. Alifanya kazi makampuni makubwa mf IBM nk. akwa anasema niligundua siwezi kuwa President akaacha, akaend akampuni nyingine vilevile akaacha kwa sababu hiyohiyo. Alipokuwa na umri wa miaka 37 akaamua kuacha kazi zote akaanza shughulizake binafsi. Na toka wakati huo hajawahi kuludi nyuma. NA sasa biashara zake zina mtaji wa Dola Ml.3 za kimarekani. almost 4.5 billion kwa hela za madafu.
Sasa basi angalia Business Plan yako for the next 3 to 5 years. Tengeneza Income Statement Projection for that period.. na kwa kuwa umekuwa nayo tayari haitakusumbua kujua Annual Revenue generation na expenses zake. Pili angalia Balance Sheet yako inasemaji in terms of equity( chako ni kiasi gani na Benki ama business patner wako) Alafu mwisho Cash flow kwa kipindi chote cha miaka utayoamua.
Hii itakusaidia kujua ni faida kiasi gani unapata kwa mwaka, hata kwa mwezi. Then hapo utakuwa na uhakika wa kujua kuwa biashara itaendelea ama lah.. Kinachoshinda wengi ni kutosimama kwa misingi ya biashara aliyoweka mwenyewe.
UKiweza kuwa na business plan nzuri na ukaisimamia basi hutokuwa na hofu ya kuacha hiyo kazi unayofanya
Option nyingine unaweza endelea na kazi yako lakini ukai monitor kwa results produced kwa uliowaajiiri but business plan ni muhimu mkuu.
All the best