Nataka kuamia dar,naomba ushauri wako wewe mkazi wa dar

Marire

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2012
Posts
12,333
Reaction score
5,292
Heshima mbele wakuu.
_Nimekuwa najishughulisha na biashara huku shinyanga kwa muda sasa ila kwa hapa nilipofikia matumaini yametoweka na naona giza mbele.
kipindi cha nyuma nilifanikiwa kununua kiwanja kama heka tatu hivi kibaha na nikajenga hapo kibanda .
sasa kwa mawazo niliyonayo kuna asseti ninazo hapa lazima niziuze na nategemea kupata kama 15m +.
na nilikuwa na wazo nikiamia dar nikafuge tu labda nifungue na duka mahala.
_sijui ni mifugo gani inalipa dar na changamoto zake na hata hilo duka sijui ni maeneo gani nikafungue.
_nimeandika uzi huu ili kupata mawazo kwenu ili nijue pa kuanzia.
Nb :nina mke na watoto watatu wawili wapo primary na mmoja miaka 3 .
 
Weka ngombe kama wewe utasimamia. Kuku kama mama anasimamia. Hivi utapata hela ya kula na mahitaji ya familia fees, ujenzi kidogo. Duka inategemea unataka kuuza nini? Kwenye kiwanja chako huwezi kuweka duka ukauza? La pangisha fremu location jirani uuze vifaa vya ujenzi, nafaka au vyakula. Kwa mtaji wako na umbali wako na mjini sidhani kama duka kkoo itakufaa na sio busara kukopa ukafungue duka. Au tafuta kibaha mjini kabisa.
 
Mama Joe kama unaishi dar nategemea utakuwa msaada kwangu.
kiwanja kilipo ni ndani kidogo kama km 1hivi..
ila najiuliza nikinunua ngombe wawili wa maziwa,hayo maziwa nitauza wapi na majini nitapata wapi?
_swala la duka hata nikifungua mbali sidhani kama itanipa shida.
 
Last edited by a moderator:
Maziwa hapa kbh unaza kuna maduka wauzaji wadogo wanaleta maziwa kila siku
Hapa kwaufugaji hasa ndio pazuri fuga kuku wengi kisha tafuta eneo kata kibali cha mbao unaweza anza na mtaji wa fuso moja inalipa unafata mafinga

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Maziwa Kibaha utauza tu soko lipo. Eneo eka tatu mvua za mwisho mwisho panda majani na miti ya kulishia mifugo, calliandra na miti mronge. Mengine huwa wanauza barabarani, fuga na kuku hata wa kienyeji. Duka mbali foleni itakugharimu muda na usafiri hivyo kuondoa umakini kwa miradi hapo home na hilo duka. Usiwaone wafanyakazi wanaoenda mjini wanasinzia na sanasana wanasubiria muda ufike wawahi foleni, sasa wewe mwenye biashara itakuwaje? Pishana na foleni hizo. Kibaha ni mji unakua haraka vifaa kama aliesema mbao utauzia wengi huku ukifatilia mifugo yako bila gharama. Usijefilisika ukakosa hata nauli kwenda dukani mjini, uko utatanuka baadae.
Mama Joe kama unaishi dar nategemea utakuwa msaada kwangu.
kiwanja kilipo ni ndani kidogo kama km 1hivi..
ila najiuliza nikinunua ngombe wawili wa maziwa,hayo maziwa nitauza wapi na majini nitapata wapi?
_swala la duka hata nikifungua mbali sidhani kama itanipa shida.
 
Last edited by a moderator:
Weka ngombe kama wewe utasimamia. Kuku kama mama anasimamia. Hivi utapata hela ya kula na mahitaji ya familia fees, ujenzi kidogo. Duka inategemea unataka kuuza nini? Kwenye kiwanja chako huwezi kuweka duka ukauza? La pangisha fremu location jirani uuze vifaa vya ujenzi, nafaka au vyakula. Kwa mtaji wako na umbali wako na mjini sidhani kama duka kkoo itakufaa na sio busara kukopa ukafungue duka. Au tafuta kibaha mjini kabisa.
Mama Joe ushauri mzuri sana huu kwa Marire

Ninauhakika Marire ukinunua ng'ombe wawili breed nzuri ukawatunza kwa uangalizi wako mwenyewe utaweza kupata returns ambazo ukilinganisha na costs unapata faida ..... hakikisha matunzo yanazingatiwa hii ni pamoja na banda, chakula na matibabu .... kidogo kidogo utaweza anza pia kuingiza mbuzi wenye maumbo makubwa .... kawaida pia mbuzi hawana gharama katika ufugaji wake kama mbuga ya malisho ipo .... na mbuzi watabakia kama liquid asset pale unapohitaji kipato cha dharura unauza ..... hii pia haikuzuii kufanya shughuli nyingine za kuingiza kipato cha kila siku ..... maziwa yatakufanya uwe na daily income to sustain your family needs
 
Last edited by a moderator:
njoo tena karibu sana, fanya biashara yoyote ile hapa dar inalipa, ila simamia mwenyewe labda ikishasimama na ukijua mzunguko kamili ndipo uwaweke watu kwa kuandikishana mkataba, huo mtaji ulionao ni mkubwa sana, watu wanatoka hata kwa kianzio 300,000/= hapa dar, ni kufanya mwenyewe na mkeo kwanza ndio utaona faida
 
wakuu nafuatilia ushauri wenu na nitaufanyia kazi...
shukrani sana
 
kuwa makini huku Dar kuna watu kazi yao ni kuibia na kuwatepeli wenzao hasa wageni, wanatumia mbinu ambazo hata wewe hautaamini kama umetapeliwa peupe
kuwa makini mkuu!!!
 
Heshima mbele wakuu.
_Nimekuwa najishughulisha na biashara huku shinyanga kwa muda sasa ila kwa hapa nilipofikia matumaini yametoweka na naona giza mbele.
kipindi cha nyuma nilifanikiwa kununua kiwanja kama heka tatu hivi kibaha na nikajenga hapo kibanda .
sasa kwa mawazo niliyonayo kuna asseti ninazo hapa lazima niziuze na nategemea kupata kama 15m +.
na nilikuwa na wazo nikiamia dar nikafuge tu labda nifungue na duka mahala.
_sijui ni mifugo gani inalipa dar na changamoto zake na hata hilo duka sijui ni maeneo gani nikafungue.
_nimeandika uzi huu ili kupata mawazo kwenu ili nijue pa kuanzia.
Nb :nina mke na watoto watatu wawili wapo primary na mmoja miaka 3 .

Mkuu Mbona shinyanga ni moja ya maeneo yenye furusa nyingi sana? Tatizo letu kubwa Wa Tanzania ni kuamini kwamba mjini ndo sehemu ya kuishi, ndo sehemu ya kutokea si kweli kabisa, Mimi nina rafiki yangu mmoja ameenda sehemu fulani kachukua poli na kajenga hoteli na anafuga huko huko na wageni wakifika inabidi kwanza wakachague kuku wa kukamatwa achinjwe au unaenda unapewa ndoana unavua samaki hapo hapo na unapikiwa.

So Mafanikio yanahitaji uvumilivu na si kingine kile, bila kuwa na spirit hiyo hata Dar inaweza kuwa ngumu tu, na mafanikio hayaji tu,

Shinyanga kuna furusa nyingi sana ila najua wengi wetu tuna aamini kweny Kufungua Duka na kuweka M pesa ndo kuna mafanikio,

Bakia huko huko Shinyanga na kaa chini ujaribu kuwza unaweza fanya nini huko? Unatakiwa uone kesho, Tatizo letu tunashindwa hapo tu kwenye kuiona kesho, Wakina Thomas edsoni waliiona kesho that is why uvumbuzi wao hautakaa upotee,
 
mkuu Chasha nakushukuru kwa ushauri wako ila hapa nilipo nimeshauchoka huu mji
kiufupi nimeshakaa hapa nikapata mafanikio tele ila nikaja nikabugi kuigia kwenye magari fuso mbili zote za mizigo moja lilipata ajali likawa right off na mzigo ya watu ikaharibika na mingine kipotea bima ilikuwa ya kawaida ikibidi hasara nibebe mimi na lingine likawa la mkopo wa bank nikashidwa kulipa marejesho ikabidi bank waliuze...
tokea hapo sijasimama wanadungu na mabalaa kibao yakafuatana....
ila namshukuru Mungu kuwa ni mzima na umri bado unaniruhusu kutafuta
 
Last edited by a moderator:
mkuu Chasha kabla sijaenda dar nitakuja Arusha kwani ndio kwetu nijifunze binu za ufugaji wa kuku ndio nijiridhishe safari ya dar ama la
 
Last edited by a moderator:
mkuu Chasha nakushukuru kwa ushauri wako ila hapa nilipo nimeshauchoka huu mji kiufupi nimeshakaa hapa nikapata mafanikio tele ila nikaja nikabugi kuigia kwenye magari fuso mbili zote za mizigo moja lilipata ajali likawa right off na mzigo ya watu ikaharibika na mingine kipotea bima ilikuwa ya kawaida ikibidi hasara nibebe mimi na lingine likawa la mkopo wa bank nikashidwa kulipa marejesho ikabidi bank waliuze...
tokea hapo sijasimama wanadungu na mabalaa kibao yakafuatana....
ila namshukuru Mungu kuwa ni mzima na umri bado unaniruhusu kutafuta
pole sana Mungu atakusimamia, ila hata Kibaha sio mjini kivile, lakini nafikiri kama nilivyosema mwanzo duka mjini kuanzia haitakufaa hadi uwe stable na kuyasoma mazingira. Kkoo kodi tu inaanzia laki 6 kuendelea kwa mwaka mzima itakata mtaji nusu. Bidhaa zinazouza labda spare mavazi wanafuata nje napo zinafanana kutoka kazi. EFD ndo hizo kodi juu ya kodi mapato hamna. Maandamano na misongamano watu hawaendi sana huko siku hizi. Hapo hujaweka wizi na utapeli risk ni kubwa mtu unayeanza.
Nakushauri ulipo ni eneo zuri tu angalia fursa hapo. All the best.
 
Last edited by a moderator:
mkuu Chasha nakushukuru kwa ushauri wako ila hapa nilipo nimeshauchoka huu mji
kiufupi nimeshakaa hapa nikapata mafanikio tele ila nikaja nikabugi kuigia kwenye magari fuso mbili zote za mizigo moja lilipata ajali likawa right off na mzigo ya watu ikaharibika na mingine kipotea bima ilikuwa ya kawaida ikibidi hasara nibebe mimi na lingine likawa la mkopo wa bank nikashidwa kulipa marejesho ikabidi bank waliuze...
tokea hapo sijasimama wanadungu na mabalaa kibao yakafuatana....
ila namshukuru Mungu kuwa ni mzima na umri bado unaniruhusu kutafuta

Dah Pole sana mkuu ila ndo Changamoto zenyewe, Ila hata kama unataka kufuga mkuu Bado hata Shinyanga unaweza fuga na bado ukafanikiwa, Unaweza fuga Kuku na unaweza fuga Ng'ombe, Ukifanikiwa kupata Breed moja kutoka Kenya ya FRECKVIEH hiyo ni balaa tupu Wasukuma ni lazima wakutafute usiku namchana, ni breed ambayo unaweza kuwa unaweza kuwa unafanya crossing huko, hii breed uzao wake wa pili hutoa hadi 45 liters za maziwa na uzao wake wa kwanza hutoa lita 38 ambapo hukamuliwa mara tatu kwa siku, Asubuhi lita 12 mchana lita 12 na jioni lita 14.
 
Mkuu Mbona shinyanga ni moja ya maeneo yenye furusa nyingi sana? Tatizo letu kubwa Wa Tanzania ni kuamini kwamba mjini ndo sehemu ya kuishi, ndo sehemu ya kutokea si kweli kabisa, Mimi nina rafiki yangu mmoja ameenda sehemu fulani kachukua poli na kajenga hoteli na anafuga huko huko na wageni wakifika inabidi kwanza wakachague kuku wa kukamatwa achinjwe au unaenda unapewa ndoana unavua samaki hapo hapo na unapikiwa.

So Mafanikio yanahitaji uvumilivu na si kingine kile, bila kuwa na spirit hiyo hata Dar inaweza kuwa ngumu tu, na mafanikio hayaji tu,

Shinyanga kuna furusa nyingi sana ila najua wengi wetu tuna aamini kweny Kufungua Duka na kuweka M pesa ndo kuna mafanikio,

Bakia huko huko Shinyanga na kaa chini ujaribu kuwza unaweza fanya nini huko? Unatakiwa uone kesho, Tatizo letu tunashindwa hapo tu kwenye kuiona kesho, Wakina Thomas edsoni waliiona kesho that is why uvumbuzi wao hautakaa upotee,

natamani nibadilishane nae yeye aje kwangu mbezichini hapa karibia na ambrosia pub mimi niende shinyanga, jamani dar inachosha na unaweza ukaja na hizo 15+m na usizifanyie kitu cha maana mpaka ukajuta, jiangalie kwanza kaka shinyanga pa zuri
 
Chasha ina maana unafuga na ngombe pia?
 
Last edited by a moderator:
Dah Pole sana mkuu ila ndo Changamoto zenyewe, Ila hata kama unataka kufuga mkuu Bado hata Shinyanga unaweza fuga na bado ukafanikiwa, Unaweza fuga Kuku na unaweza fuga Ng'ombe, Ukifanikiwa kupata Breed moja kutoka Kenya ya FRECKVIEH hiyo ni balaa tupu Wasukuma ni lazima wakutafute usiku namchana, ni breed ambayo unaweza kuwa unaweza kuwa unafanya crossing huko, hii breed uzao wake wa pili hutoa hadi 45 liters za maziwa na uzao wake wa kwanza hutoa lita 38 ambapo hukamuliwa mara tatu kwa siku, Asubuhi lita 12 mchana lita 12 na jioni lita 14.
Hivi mkuu hii breed ukiagiza mpaka ifike bongo ina cost kiasi gani mimi ni mfugaji na demand ya soko ni kubwa kwa sasa nazalisha lita 60-80 kwa ng'ombe 7. Sasa supply imezidiwa kwa sasa nahitaji lita 150 kila siku. Nilikuwa naangalia option ya kupata ng'ombe wa aina hii ili niongeze uzalishaji. Naomba unisaidie kama unajua gharama hiyo breed kule inauzwaje na gharama ya usafirishaji au ni wapi kwa hapa Tanzania naweza ipata hiyo breed
 
Mkuu kwa Tanzania walikuwa hawajafika, kenya kwenyewe hana muda, hii ukiwa na wawili karbia lita 100, kusafirisha hadi Dar ni ishu optional ni kununua mbegu
 
Back
Top Bottom