Nataka kuanza kuuza mchele jumla na reja reja

Nataka kuanza kuuza mchele jumla na reja reja

Frank silva

New Member
Joined
Oct 26, 2019
Posts
2
Reaction score
0
Wadau ipi inalipa kati ya kununua shambani then ukoboleshe na kuupeleka dukani au kununua tu mashineni moja kwa moja nakuenda kuuza dukani. Ipi iko sawa zaidi? Na je, mgawanyo wafaida ukoje kwa wazoefu?
 
Bora ununue mashineni upeleke sokoni kununua shambani mpunga inahitaji umakini wa hali ya juu kuanzia kukagua mpunga kama mzuri,upimaji nao lakini Michele unauona kikubwa kama ni Michele itakuhitaji ujue solo lako yule final consumer ni wa Michele super au wa kati mfano huku mngeta-Ifakara Michele mpaka 1250 wa kawaida unapata.
 
Ni biashara nzuri na inalipa, kwa kuwa mchele ni moja ya bidhaa inayohitajika kila siku. Muhimu uwe na anuani rasmi ambapo wateja wako wanaweza kukupata, mchele uwe na kiwango cha juu (grade one), bei iwe rafiki (pengine fanya iwe chini kuliko wauzaji wengi kwa maeneo unayouzia).

Pia, ongeza jitihada kutafuta masoko kwa wenye uhitaji, mfano mahoteli, restaurant, migahawa, kumbi za sherehe, supermarkets, nk bila kusahau matangazo ya kutosha.
 
Hii biashara mkuu hata mm nawaza niianze mwaka huu,biashara hii inalipa vizuri na hautakaa na mzigo muda mrefu sababu ni vitu vinavyohitajika kila siku majumbani

Ila nakushauri ni vyema uanze kipindi cha mavuno kwa wakulima na uende ukanunue huko,utapata kwa bei rahisi sana na utauza kwa bei nzuri lkn jitofautishe na wauzaji wengine punguza bei usitake faida kubwa

Mwisho kama una uwezo unaweza ukatafuta mashamba ukaanza kulima mwenyewe

Kuna kijiji nilienda kumsalimia mamdogo wangu nikakuta watoto wako std7 lkn wana maisha yao tayari kwa kutegemea huu ubwabwa,wamenitia hasira sana nami nianze kupambania huko..

Ukianza tushauriane hata mawazo,utafika mbali mkuu usirudi nyuma ktk hilo wazo
 
nakushauri ujue kwanza kuandika vizuri ndio uanze biashara, kwa mtindo huu utatapeliwa na kufirisika haraka sana
Hapana mkuu kuandika vizuri na hiyo biashara na kutapeliwa ni vitu tofauti,,ajikaze tu hii biashara atatoboa
 
Back
Top Bottom