Wapendwa sana wanaJF, habari za asubuhi...
Siku chache zijazo nimefikiria kuanzisha biashara ya kuuza soda za chupa na za kopo (take away) kwa bei ya jumla na rejareja.
Mwenye uzoefu na biashara hii naomba anijuze kuhusu mtaji, faida na changamoto za biashara hii. Aidha kama kuna maujanja mengine kuhusu biashara hii anijuze.
Nitashukuru kwa msaada wenu.

Kwema mdau, biashara ya soda ni nzuri iwapo ukipata sehemu nzuri ya mzunguko wa watu na pia Mimi nitatoa gharama za rejareja kuhusu biashara iyo ya soda.
Ukinunua being jumla kwa wakala wa vinywaji Bei zake ni kama ifuatavyo
1. Pepsi - 20,000/= (kreti ikiwa na soda zake) ila kama una kreti yako utabadilisha/kununua kwa 9,800/=.
2. Cocacola- 20,000/= (kreti ikiwa na soda zake) ila kama una kreti yako utabadilisha/kununua kwa 9,800/=
3. Jambo soda, energy & juice 300ml -4,500/= per katoni
4. Jambo maji 1.5ltr - 4,000/= per katoni
WwwWw
5. Jambo Maji 500ml - 3,500/= per katoni
Faida zake ni:-
1. Pepsi (Ina chupa 24) - 2,200/= per kreti moja.
2. Coca-Cola (Ina chupa 24) - 2,200/= per kreti moja.
3.Jambo soda, energy & juice (zipo chupa 12 kwa Kila katoni) - 1,500/=
4. Jambo maji 1.5 lita (ina chupa 6) - 2,000/= kwa katoni moja.
5. Jambo maji 500ml (chupa 12) - 2,500/= kwa katoni.
NB:- hizo ni gharama za kununua vinywaji kwa Bei ya jumla toka kwa mawakala na ukauza kwa rejareja ila gharama hutofautiana mkoa kwa mkoa.
Na pia fremu gharama zake hutofautiana mkoa kwa mkoa ila ukiwa na kianzio cha laki 3 unafanya biashara vizuri tu chunguza Kwanza kabla hujaanza.