mwanachondogoro
Member
- Aug 27, 2013
- 40
- 8
Zanzibar kuna vituo viwili vya msaada wa kisheria ZANZIBA LEGAL CENTER na ZAFELA hiki ni chama cha wanawake wanasheria lakini kwa uzoefu wangu ivi vyote havina msaada sana katika jamii kwa sababu wote wanaofanya kazi katika vituo hivyo wengi wao si mawakili kwahiyo hata kama watampa mtu msaada wa kisheria basi mengi ni maneno tu na wakimsaidia sana watamuandikia mtu hati ya madai halafu hawawezi kumsimamia mahakamani na hati zenyewe za madai mara nyingi zinapigwa na chini tu kwa pingamizi za awali kwa sababu hazikidhi viwango vya kisheria. Pili imekuwa nafaya kazi na chemba moja hivi kwa muda mrefu na malipo yake ni kama najitolea tu sasa nikapata wazo kama hapa najitolea kwanii nisianzishe tu kituo cha msaada wa kisheria ili iweze kusaidia watu tu moja kwa moja kuliko kuendelea kumfaidisha mmiliki wa chemba na mkooni nina kama million mbili za kuanzia plz wanasheria wenzangu naomba mawazo yenu jinsi gani nifanye ili niweze kufanikisha zoezi hili kwa taarifa tu nimeshafanya utafiti wa kutosha na nahisi inawezekana nahitaji tu kupata mawazo zaidi kutoka kwenu.