Nataka kuanzisha kituo cha msaada wa kisheria zanzibar

Joined
Aug 27, 2013
Posts
40
Reaction score
8
Zanzibar kuna vituo viwili vya msaada wa kisheria ZANZIBA LEGAL CENTER na ZAFELA hiki ni chama cha wanawake wanasheria lakini kwa uzoefu wangu ivi vyote havina msaada sana katika jamii kwa sababu wote wanaofanya kazi katika vituo hivyo wengi wao si mawakili kwahiyo hata kama watampa mtu msaada wa kisheria basi mengi ni maneno tu na wakimsaidia sana watamuandikia mtu hati ya madai halafu hawawezi kumsimamia mahakamani na hati zenyewe za madai mara nyingi zinapigwa na chini tu kwa pingamizi za awali kwa sababu hazikidhi viwango vya kisheria. Pili imekuwa nafaya kazi na chemba moja hivi kwa muda mrefu na malipo yake ni kama najitolea tu sasa nikapata wazo kama hapa najitolea kwanii nisianzishe tu kituo cha msaada wa kisheria ili iweze kusaidia watu tu moja kwa moja kuliko kuendelea kumfaidisha mmiliki wa chemba na mkooni nina kama million mbili za kuanzia plz wanasheria wenzangu naomba mawazo yenu jinsi gani nifanye ili niweze kufanikisha zoezi hili kwa taarifa tu nimeshafanya utafiti wa kutosha na nahisi inawezekana nahitaji tu kupata mawazo zaidi kutoka kwenu.
 
Unaweza kuanzisha kama NGO tu ukiwa na brand ya kutoa legal aid, hivyo fuata sheria za uanzishaji wa NGO hapo Zanzibar kama unahisi una mandate, capacity na kuna hiyo demand, kimsingi, Legal AID Centre kama ilivyo NGO nyengine sio mali binafsi ni public entity hivyo usieme nataka kuanzisha as if it is a company, you just hold a generic idea ambayo inatakiwa kuungwa mkono na watu ambao watakua ndio alliance mwenye wako ku support idea yako na ndivyo ilivyo as a legal requiremen, kwa Tanganyika huku mnatakiwa kuwa zaidi ya 8 kama sikosei kuanzisha NGO, zaidi wasiliana na hizo existing upate mawazo zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…