Kwanza hongera kwa kuwaza kijasiria mali.
Pili, hakuna biashara isiyo na changamoto otherwise kila mtu angekuwa tajiri. Tofauti kati ya maskini na matajiri ni matajiri kuhimili changamoto. Jitume mkuu.
Tatu, changamoto ya kwanza ni wewe kutofahamika maana hujajieleza vya kutosha.Wewe ni nani na jamii inakujua. Kwamba wanakujua au la si hoja. Biashara unaweza ila ukijulikana let say mwl wa Chuo x unakuwa na faida zaidi kuliko anayeanza - japo mwisho wa siku wote mtafanikiwa.
Nne, training inatakiwa wewe mwenyewe uwe na mvuto. Kuwa na mvuto siyo sura. Lazima uwe msomaji wa vitabu vingi sana. Ile taarifa zako ndo mvuto. Kisha ndo unawatafuta wengine kujazia maeneo mengine ambayo wewe siyo mtaalam.
Tano, tafuta mshauri hata kama hana centa kama yako. Badilshana mawazo na watu wengi itakusaidia.
Mwisho, tafuta kitbu kinaitwa rich dad poor dad, itakufanya ukaze mwendo. Ajira siyo deal siku hizo.
kila la kheri.