Nataka kubadili engine ya gari aina ya Isuzu bigon, ili niweke engine nyingine tofauti

Mkuu gear box yako ni auto au manual? Je kama ni auto inakubari kufika speed 120km/h? Je baada ya kubadilisha engine rpm inasoma vizuri,maana, mkuu hata mimi nina mpango huo wa kubadilisha engine pindi hii 4jx1 itakapo dead.
Ipo fresh boss, rpm haikua inafanya kazi toka mwanzo na sijahangaika nayo baada ya kubadili engine. Kwa speed ipo poa. Nilienda nayo tukuyu. 120-140km/h ni kawaida.

Gali imenisumbua kinoma ila ndio ivyo tena nina mahaba nazo. Kuna moja nimeiona i wish to have it. Mambo ya engine nishajua jinsi ya ku deal nayo
 
Asante sana ndugu, ulibadilishia garage ipi? Halafu pia hiyo 4jg2 ni lazima iwe yenye manual injector pump? au ya electronic injector pump?
 
Sasa si mateso hayo, gari yako unakuwa kama umeiiba bana😂😂😂
 
Isuzu wana design body nzuri hasa wizard naikubali sana iwe V6 petrol ila hayo majanga ya engine sikuwahi kuyajua
 
ISUZU Trooper imeminywa ubavuni toka lini?
Basi hutakuwa hio gari huijui vyema kuna namna imeminywa body katikati ya milango. Kulekea mpaka kwenye taa ya nyuma. Ule mkunjo haunivutii hata kidogo
 
Mkuu unapatikana wapi? Nahitaji msaada wako kwenye hii issue
 
Unahitaji msaada gani kwenye Isuzu?
Yes Mkuu Nina Isuzu Trooper ya 2001 niliinunua hivi karibuni Ina Engine ya 4JX1 Manual gearbox. Tatizo LA hii Engine ni kwamba haikimbii zaidi ya 60kph. Yaani ukiwa Silence ukikanya mafuta RPM inapanda vizuri tu lakini ukiwa unaendesha hata ukanyage throttle hadi mwisho Haikimbii zaidi ya 60kph RPM inakwamia kwenye 2.9 hivi na matokeo yake nguvu inakuwa ndogo kwenye higher gear na mafuta yanatumika sana kwa sababu kilima kidogo inabidi uende hadi 2 au 1 kabisa. Tatizo ni lipi? Najua hizi Engine ni Nzuri ile nimekwama hapo.
Kuna kipindi ilichemsha nikachonga Cylinder head lakini ikadevelop Hilo tatizo. Sawa nimekwamia hapo
Sina hakika kama bongo Kuna fundi wa hizi Engine Mwenye Tech02 msaada wako kwenye hii ni muhimu mkuu
 
Nakucheki inbox
 
Ni sawa na mwanaume kutaka kubadilisha jinsia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…