Nataka kufa njaa na Dollar za Zimbabwe.

Eraldius

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2011
Posts
1,122
Reaction score
912
Mwenye kujua. Wapi wanafanya Exchange ya hizi pesa hapa Mwanza? Nisaidie
 
Mkuu si kwamba kila mahali unaweza kubadilisha fedha za kigeni, na Kubadilisha fedha za kigeni kunategemeana na demand ya hizo pesa, hizo za Zimbabwe je zina demand? kuna wafanya biashara wanazihitaji kwa ajili ya kwenda kufanyia biashara zimbabwe? nazani jibu ni Hapana,

Mkuu hata pesa kama za uganda inabadilishwa Tz kwa sababu tu tuko nao jirani, vinginevyo zisingekuwa na ishu kabisa, na pesa kama za Zambia, Malawi, Rwanda na kazalika hubadilishwa mipakani, na kwa sababu zimbabwe hatupakani nayo labuda ukabadilishie mpakani mwa Zambia na Zimbabwe au nenda Ubalozi wao Dar wanaweza kukusaidia, ila kwa hapo Mwanza ni vigumu sana,
 
Hakuna dola ya Zimbabwe. **** unayo dola ya Zimbabwe fanyia kitu chochote lakini siyo kusumbuka kuibadilisha kwani haina thamani kabisa. Zimbabwe walishaitosa na sasa wanatumia US Dollar, Suid Africa Rand, Botswana Pula, n.k.
 
Mwenye kujua. Wapi wanafanya Exchange ya hizi pesa hapa Mwanza? Nisaidie

Mimi nashauri uende zimbabwe ukakae kwa muda ukitafakari nini cha kufanya ukirudi TZ.huko utatumia hizo Zimdolla kiurahisi sana
 
Dola ya Zimbabwe !!!! Hapo kweli utakufa njaa, pole sana. Hiyo hainunuliwi hapo TZ, hata Mitcasi ya jirani zako Mozambique ukiwa nazo ni bure tu !!!
 
Nashukuru kwa ushauri wenu.Ngoja nijipange.exchange rate of 27/05/2012 ZWD 1=TSH.4.18141 Ninayo ZWD 100000.
 
Nashukuru kwa ushauri wenu.Ngoja nijipange.exchange rate of 27/05/2012 ZWD 1=TSH.4.18141 Ninayo ZWD 100000.

Nakushauri usijisumbue. Hiyo pesa htaweza kununulia hata andazi mojja kule Zimbabwe kwenyewe.
 
Nashukuru kwa ushauri wenu.Ngoja nijipange.exchange rate of 27/05/2012 ZWD 1=TSH.4.18141 Ninayo ZWD 100000.

Mkuu unatuyeyusha rate ya ukweli ni hii,fungu la mchicha zimbabwe ni 100mils ZMD na kwa bongo ni sh 200Tsh kwahyo 1Tsh=500,000ZMD,kwa kukurahisishia hyo laki moja yako ya zimbabwe ni sawa ni Shillingi tano ya Tanzania sasa sijui utanunua nini maana hata big G sh 50Tsh.
 
Hizo ulitakiwa uziache Airport ungetoa TIP kwa wafanyakazi pale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…