Nataka kufanya biashara ya kukoboa mpunga na machine za kisasa kama za kichina

Nataka kufanya biashara ya kukoboa mpunga na machine za kisasa kama za kichina

Bukali

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2018
Posts
1,264
Reaction score
835
Ndg wanaboard, naombeni ushauri wenu maana ninawazo la biashara.

Nipo Geita, mtaji nilio nao ni 25M, nimepata machine ya kukoboa 25t/h, ya Kisasa.

Ambayo wanauza 8700usd. Inakuwa na:

1. Elevators zake 2
2. Destoner
3. Cleaner.

Pia inaoption ya kupata brown rice.

Shida yangu ni ushauri, je nichukue hii ama ni chukue zile za kizamani ambazo ni kinu pekee. Naombeni sana ushauri wenu wa kujenga.

Hii nyeupe na green ndo 8700 USD.
IMG-20210404-WA0010.jpg
Wanabod ndo hizo hapo sasa.

Hii ni 6000USD
IMG-20210420-WA0013.jpg
 
Mkuu chukua hiyo machine ya 8700 usd, dunia sasa inaenda na technology, achana na mashine za kizamani zitakukwamisha, 2700 usd isije ikakupa taabu na majuto.
 
Location ndio inayoamua, kama unaweza kufanya kazi kubwa chukua ya mwanzoni. Lakini kama eneo ni lile la kazi za debe sijui kilo 50 basi uchukue yenye kinu pekee maana usije ukawa sawa na kununua basi na kulipeleka eneo lenye abiria watatu kwa siku.
 
Chukua hiyo ambayo inaweza kutenganisha Birian maana mchele wa birian ni tatizo kwenye hiyo biashara.
 
L
Location ndo inayoamua, kama unaweza kufanya kazi kubwa chukua ya mwanzoni. Lakini kama eneo ni lile la kazi za debe sijui kilo 50 basi uchukue yenye kinu pekee maana usije ukawa sawa na kununua basi na kulipeleka eneo lenye abiria watatu kwa siku.
Location ipo powa sana.
 
Hiyo ya USD 8700 nzuri Sana na itakulipa. Kuna maeneo uhitaji ni mkubwa sana! Kuna sehemu inaitwa mlowo mbozi huko mkoa wa songwe pale mashine kubwa ya hivyo hamna zipo za vinu na chache alafu ukizingatia hapo ndio njia yanapita magari yanayotoka sehem inaitwa kamsamba ambako unatoka Mchele Safi Sana ukitoa kyela huko ndo Kwa pili Kwa Mchele Bora. Ko ukitega pale utapiga Sana pesa.
 
Naomba wataalamu wa kuagiza vitu kutoka China.
 
Ndg wanaboard, naombeni ushauri wenu maana ninawazo la biashara.

Nipo Geita, mtaji nilio nao ni 25M, nimepata machine ya kukoboa 25t/h, ya Kisasa.

Ambayo wanauza 8700usd. Inakuwa na:

1. Elevators zake 2
2. Destoner
3. Cleaner.

Pia inaoption ya kupata brown rice.

Shida yangu ni ushauri, je nichukue hii ama ni chukue zile za kizamani ambazo ni kinu pekee. Naombeni sana ushauri wenu wa kujenga.

Hii nyeupe na green ndo 8700 USD.
View attachment 1765108Wanabod ndo hizo hapo sasa.

Hii ni 6000USD
View attachment 1765115
Mkuu mimi nakujibu kulingana na uzoefu wangu upande wa spare za mashine gani na watu wengi wananiagiza China.

Kama uko eneo la biashara na uhitaji wa machine kubwa kiasi cha watu kupanga foleni,capital ipo na uhakika wa spare + mafundi Chukua mashine ya kwanza,haitakuangusha kulingana na uwezo wake.

ila kama upo sehemu yenye uhitaji wa machine wa kawaida,nenda na chaguo lapili.Ile bila shaka ni SB50.Nina agiza spare zake nyingi kila mara hiyo inaniaminisha watu wengi wanatumia hizi mashine.Hivyo itakuwa ni rahisi kwako kupata spare na mafundi.
rubber rollers

rubber rollers.png

14 inch.jpg

Screens (chekeche)
screens.jpg

screen.jpg

Kila la heri mkuu

rubber.jpg
 
Hiyo ya USD 8700 nzuri Sana na itakulipa. Kuna maeneo uhitaji ni mkubwa sana! Kuna sehemu inaitwa mlowo mbozi huko mkoa wa songwe pale mashine kubwa ya hivyo hamna zipo za vinu na chache alafu ukizingatia hapo ndio njia yanapita magari yanayotoka sehem inaitwa kamsamba ambako unatoka Mchele Safi Sana ukitoa kyela huko ndo Kwa pili Kwa Mchele Bora. Ko ukitega pale utapiga Sana pesa.
Mkuu kyela siku hizi hawana mchele mzuri walishaanza kulima kwa mbolea wale.
Mchele mzuri sasa hivi upo Kamsamba na Rukwa tu alaf Mlowo sasa hv kuna matajiri wamefunga mashine za kisasa sana na wanazid kufunga.
 
Yote sawa ila mimi nadhani hiyo mashine inaweza kufungwa POPOTE hapa nchini ili mradi kuwe na uwezekano wa kupata mchele, uwe wa Kyela, Mbeya, Kamsamba au hata Rukwa! Ili mradi malighafi hiyo ifike kwenye mashine na machakato uendelee. Hivyo ifunge hata Dar na uletewe huo mchele uuchakate na kisha uupaki na uuze hapa Dar au hata nje, huko Kenye, Rwanda, Burundi hata Sudani Mpya! Wenye mihela yenu jaribu KU THINK NJE YA BOKSI!
 
Back
Top Bottom