Nataka kufuga bundi, lakini jamii hainielewi

Nataka kufuga bundi, lakini jamii hainielewi

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
1712772320881.png


Nataka kufuga bundi kuzuia uharibifu wa panya wa mazao shambani kwangu, ila sasa hii jamii ninayoishi nayo wakiona nakusanya bundi hawanielewi, wanadhani mie mchawi. Halafu mie nawaona bundi wako wa-cute!

Nifanyeje? Wasije wakanichoma moto ndani ya nyumba yangu.
 
Tafuta njia nyingine ya kupambana na hao panya badala ya kupambana na jamii inayokuzunguka.
 
Ni wajibu wako kuprove kwenye jamii yako kuwa bundi ni ndege kama ndege wengine.
 
Wewe fuga tu. Nitakuwa mteja wako wa mayai. Nasikia ni matamu sana ukiyakaanga.
 
Bundi hafugiki fugiki tu mkuu,mpaka upate chaneli.Wengi walio mjini Wana watu,so usiende kujitegea bundi mtaani yatakukuta.Halafu aliyekwambia bundi anapenda panya ni nani?Ndio anakula ila kupenda kula Hilo ni jambo lingine,so leave bundi alone,maana hata mm nahisi unataka anza ulozi.
 
Back
Top Bottom