Nataka kufuga kuku chotara,naomba maelezo

Marire

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2012
Posts
12,333
Reaction score
5,292
Heshima kwenu wakuu.
Nimetegeneza bada la kutosha kuku kama 30+ nia yangu ilikuwa nifuge kuku wa kienyeji na kuna mtu ameniahidi kuniletea toka shinyanga vijijini kwa 5000@ na nilipanga nianze na majike 10 na jogoo 1 .
ila sasa nimevutiwa na yale makuku chotara makubwa kubwa hivi nataka kujua ni wepi rahisi kufuga na wastahimilivu wa magonjwa?
Naomba mawazo yenu ikiwa ni pamoja vitabu gani vizuri ninunue kwa ajili ya ufugaji wakuku
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
NB: kuna ulazima kuwafungulia kuku kula nje ya banda na kutowafungulia watakosa nini katika miili yao?
 
Swala la kuku wanao stahimili magonjwa kwa kweli ni swala gumu sana na asikudanganye mtu, Kuku wa kienyeji huwa wanakufa kama kawaida ingawa watu wanadhani ndo wanastahimili magonjwa.
Kinacho takiwa ni kufuata kanuni za ufugaji, huwezi acha kufuata kanuni halafu ujidanganye kuna kuku wanasthimili magonjwa, wewe fuata kanuni zote na kuku wako hawatakufa hovyo ila usipo fuata hakuna cha aina ya kuku wanakufa tu.
 
chotara......si mweusi wala si mweupe!

ni pm au nitumie email yako nikutumie info on poultry
 
kesho natengeneza email then nitakutumia mkuu wangu
 
Swala la kuku wanao stahimili magonjwa kwa kweli ni swala gumu sana na asikudanganye mtu, Kuku wa kienyeji huwa wanakufa kama kawaida ingawa watu wanadhani ndo wanastahimili magonjwa.
Kinacho takiwa ni kufuata kanuni za ufugaji, huwezi acha kufuata kanuni halafu ujidanganye kuna kuku wanasthimili magonjwa, wewe fuata kanuni zote na kuku wako hawatakufa hovyo ila usipo fuata hakuna cha aina ya kuku wanakufa tu.

umeongea ya
maana sana mkuu
 
Jambo la msingi ni kuwapa chanjo kama ni vafaranga ama unavyowapokea tu..hapo utawakinga na magonjwa kwa kiasi kikubwa
Heshima kwenu wakuu.
Nimetegeneza bada la kutosha kuku kama 30+ nia yangu ilikuwa nifuge kuku wa kienyeji na kuna mtu ameniahidi kuniletea toka shinyanga vijijini kwa 5000@ na nilipanga nianze na majike 10 na jogoo 1 .
ila sasa nimevutiwa na yale makuku chotara makubwa kubwa hivi nataka kujua ni wepi rahisi kufuga na wastahimilivu wa magonjwa?
Naomba mawazo yenu ikiwa ni pamoja vitabu gani vizuri ninunue kwa ajili ya ufugaji wakuku
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
NB: kuna ulazima kuwafungulia kuku kula nje ya banda na kutowafungulia watakosa nini katika miili yao?
 
Chotara ni wazuri kwani wanastahimili magonjwa na wanataga vizuri pia mayai yao yanambegu so unaweza yatotolesha kama ya kienyeji tu
 
Back
Top Bottom