Nataka kufuga nyuki kisasa

Elimu nzuri sana..unapatikana wapi??Naomba namba zako
 
Nimetoka shamba wiki hii...mizinga michache ya juu ya miti inaingia nyuki ila ya kwenye vichanja hakuna zaidi ya wadudu. Tunampango wa kuiondoa kutoka kwenye vichanja na kupandisha juu
 
Bei ya mzinga ikoje na ikibidi weka mawasiliano
 
Bado Mkuu...mizinga ilikuwa inaingiliwa na wadudu nyuki wanahama.Nimebadilisha fundi na tunaambika tena ambayo haina nyuki
Mkuu mimi nilianza kufuga nyuki kwa mizinga 20 mwaka 2020. Somo kubwa nililojifunza nyuki hawapatani kabisa na wadudu, hivyo ibabidi angalau kila mwezi ukague mizinga na kusafisha wadudu angalau mara 2 vingunevyo nyuki hawaingii au hukimbia. Ila sasa niko busy sana sipati muda wa kutosha kuifuatilia. Ndio shida huanzia hapo.
 
Nimetoka shamba wiki hii...mizinga michache ya juu ya miti inaingia nyuki ila ya kwenye vichanja hakuna zaidi ya wadudu. Tunampango wa kuiondoa kutoka kwenye vichanja na kupandisha juu
Moja: Ukiwa na Kichanja au Kibanda, hakikisha unatega Nyuki nje (kwenye miti) kisha iliingia Nyuki ndipo uihanishie kibandani.

Nyuki hawawezi kuingia kwa wingi kibandani na kwa haraka kama kwenye miti.
Mbili: Kibanda au Kichanja lazima miguu yake inayogusa ardhi iandaliwe kudhibiti wadudu kama siafu na sisimizi n.k
Pichani chini ni moja kati ya vibanda cha Mizinga 48 tunavyotayarisha kwa nguzi za chuma na kila nguzi kujengewa eneo la kuwekewa oil kuzuwia wadudu lakini pia kusakafiwa chini hivyo kuzuwia Majani Kuota ambayo ni chanzoncha wadudu.
 

Attachments

  • IMG_20241022_144711.jpg
    1.4 MB · Views: 1
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…