Wakuu heshima kwenu.
Naombeni ufafanuzi na maelekezo ya kufata Ili kufunga MITA ya luku inayojitegemea.
Je hatua gani za kufata?
Vitu gani vinahitajika?
Gharama ya mchakato mzima ikoje??
Asanteni sana.
TANESCO
Mpendwa Mteja !
Zifuatazo ni gharama halisi za kuunganishiwa umeme kuanzia tarehe 5/01/2022
[emoji3578]Gharama za kuunganisha umeme
mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia moja kutoka kwenye miundombinu ya umeme ni
shilingi 320,960/=,
[emoji3578] Mteja wa njia moja
ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme
shilingi 515,618/=,
[emoji3578]Umbali wa njia moja
ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme
shilingi 696,670/=
[emoji3578]Aidha, gharama za kuunganisha umeme
ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia tatu kutoka kwenye miundombinu ya umeme
shilingi 912,014/=,
[emoji3578] Mteja wa
njia tatu ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme
shilingi 1,249,385/=,
[emoji3578]umbali wa
njia tatu ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme
shilingi 1,639,156/=.
Zingatia
Gharama ya kuunganisha umeme
vijijini kwa wateja wa njia moja ni shilingi 27,000/= kama ilivyoelekezwa na EWURA.
NB: Gharama zote zimejumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).