Nataka kufunga ndoa bila sherehe

MENISON

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2013
Posts
726
Reaction score
621
Hii imekaaje wazee mwezi December nataka kufunga ndoa KKKT Mbezi Dar. Sasa watu wananishangaa kwanini sichangishi na wala siwaambii.

Mchungaji wangu ameniambia kazi yake ni kufungisha ndoa hayo ni ziada,
Hii imekaaje? Au mimi ndio wa kwanza kufanya hivi?
 
Inawezekana mkuu, Mimi nikikumbuka yakwangu mbaka nacheka.
Nilishtukizatuu watu wakashangaa ninafungandoa wakaja kanisani ilenatokatu naingia kwenye kimeochangu na wife naona watu rundo wananipigia vigelegele na magari yananifuata sijui ilikuwaje wengine nikawakuta home dah nilishangaasana.

Walinilaumu sana, wakajichangisha michango ya gafla waka nunua gambe sherehe ikawa hapohapo nyumbani hadi saa saba usiku maana kadiri muda ulivyokuwa unakwenda ndio walikuwa wakipigiana cm na kuongezeka.
Kwakweli sikuamini.
Mimi nimchangiaji mzuri wa harusi za wenzangu lakini yangu sikutaka kusumbua mtu nikaamua kufanya kimyakimya.
 
Hutokuwa wa kwanza mzee, mwaka jana broo wangu akifunga ndoa kama hiyo, yy alienda na mashahidi tu na wakezi coz wazaz walikuwa mbali, ngoma ikaisha wakarudi home , jtatu akarudi kazini, pasaka akawakutanisha wazazi wa pande zote kwa kasherehe kadogo, maisha yanaendelea.
 
Kisheria ndoa lazima iwe na sherehe.Ingawa sheria ya ndoa haijasema sherehe iwe vipi.Kwa hiyo fanyeni sherehe hata ya watu kumi tu haina tatizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…