Nataka kufunga ndoa bila sherehe

We cio wa kwanza wala wa mwisho, lkn inategemea na maridhiano baina yako na anayeolewa. Usije ukawa una plan vyako na yy vyake
 
nina ndugu yangu akatoka kuoa juzi tu kama hivyo. alichofanya ni kutumia watu tu ujumbe kuwa jumamosi moja atakuwa anaenda funga ndoa wote wanakaribishwa.hakuna cha matarumbeta wala nini hata gari la maharusi halikupambwa! na ni mtu mwenye kipato kizuri sana tu. cha zaidi alialika marafiki zake na ndugu wa karibu baadae kwenye kitafrija kidogo ambacho aligharamikia mwenyewe. sema marafiki zake waliamua kumchangia baada ya sherehe kama zawadi tu pamoja na jamaa kukataa.


inawezekana sana boss mi mwenyewe ni muumini wa ndoa kama hizo. kila kheri mkuu.
 
Sio mbaya
Baraka za Mungu zinatosha

Kila la kheri
Sina uhakika km hii kheri umeitoa kwa moyo wote..! Wadada mnavyopenda harusi what if ungekuwa ni wewe unayeolewa??
 
Mkuu uko sahihi sana, Mimi mwenyewe tarh 28 mwezi huu nafunga ndoa kama yako, mke wangu ni mwalimu hivyo kuwachangisha watu ni kuwasumbua tu, mungu akubaliki sana mpendwa
Duh! Ngoja na mimi nikaoe aisei make kujipanga na harusi hatimaye uhenga utanikutiliza sasa..!
 
Mimi nafunga ndoa mwezi huu isee, nilikuwa nataka kufanya hii style nimemwambia wife Mimi nataka ndoa tu kanisani then tusepe zetu, ila yeye anataka sherehe nimemwambia sherehe atafanya yeye huko ukumbini Mimi kipindi hiko Niko geto, akimaliza sherehe anitafute, sipendagi usumbufu isee
 
Mkuuu unamaanisha hatutakula
Pilau
 
Ndoa ni kanisani bwana mkubwa, sherehe mbwembwe tu, na pia sherehe utasumbuka sana michango labda huwe umejipanga kifedha
 
Utaweka mfano wa kuigwa ila inabid isiwe weekend funga siku za kazi watu wapo busy hakuna wa kukufuatilia.utapunguza maneno
Hii mentality ndio inafanya watu washindwe kufanya mambo yao kwa Ufanisi zaidi; Kwanini apunguze maneno? Haina haja ya kuongopa maneno, acha afanye siku yoyote amabayo ataipenda.
 
Kisheria ndoa lazima iwe na sherehe.Ingawa sheria ya ndoa haijasema sherehe iwe vipi.Kwa hiyo fanyeni sherehe hata ya watu kumi tu haina tatizo.
Sheria ipi mkuu? Labda kwa upande mwingine; Ila kwa Wakristo hakuna Sheria; Neno la Mungu linasema ivi Ukiwa na Neema uko juu ya Sheria, Simply ni kwamba ukiwa na Neema ya Mungu Sheria haikusumbui.

Labda useme ni Sherehe ni Utamaduni na sio Sherehe ni Sheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…