Nataka kufungua Bekari

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Posts
34,181
Reaction score
41,563
Wakuu,

Kama kuna mtu yeyote anaweza kunipatia DESA - nataka kufungua bekari ya mikate.
a) Vifaa Muhimu vinavyohitajika
b) Soko la mikate nchini
c) Material yatakayohitajika
d) Changamoto
e) Mtaji - approx

Natanguliza shukrani kwenu.

Yaani hali lipofikia inabidi tuwe wajasilimali maana bila hivyo lazima ofisini udokoe tu hali ni tete.
 
mbona mmechuna -- yaani humu JF hakuna mtu anayefanya hii biashara?
 

Mkuu Hongera sana kwa hilo, Ila mimi naamini techinojia ya kutengeneza mikate ni rahisi sana na vifaa vya kuokea ukienda hata SIDO utapata vya kuanzia then mtaji ukikuwa ndo u import vifaa vikubwa kutoka nje.

1. VIFAA VYA KUTENGENEZEA- SIDO utapata vya kunazia

2. SOKO LAKE- Mkuu hapa kuna ushindani sana kutokana na kuwa na Direct and Inderct Competitors
a. Direct competitors- Hawa ni wazalishaji wa mikate na kuna viwanda vingi sana Dar na kwenye miji mingine mikubwa kama Arusha, Mwanza, mbeya, Tanga na Dodoma
b. Inderct competitors- Hawa ni watengeneza Mandazi, chapati, wakaanga mihogo, viazi, keki, vitumbua, sambusa na
kazalika
Soko la mikate huwa haliko contry wide yaani Mikate ya Dar huwezi iona Arusha na ya Arusha huwezi iona Morogoro mara nyingi hii iko kimiji sana na kimitaa
So wewe unaweza anza na mtaa wako kwanza

LAZIMA UFANYE ANALYSISI YA HAWA COMPETITITORS KWANZA UJUE NGUVU ZAO NA UDHAIFU WAO NA UJE NA MIBUNA ZA KUPAMBANA NAO

3. Materio yano hitajika
Kuna vitu vingi huhitajika na hii inategemea aina ya mikate
- Unga wa ngano
- slt
- Baking powder
- yeast
Hizo ni komoni sana

Ila mikate inaweza vile vile kujumuisha
- sugar
- eggs
- milk
- spice
- fruits
Vegtable na kazalika

4. Changamoto
- Hapa kwenye changa moto napo ina depend mkuu, na kuna kuridishiwa mikate iliyo chacha, competition, kupata vibari vya TBS, TFDA hapa ndo kuna kazi kubwa sana

5. MTAJI- Hapo sikudanganyi inategemea unaaza na ukubwa gani make kuna wanao anza hata na mikate 30, na wakisha anza ku penetrate kwenye soko wanongeza taratibu

NA KUNA INA ZAIDI YA 8 ZA MIKATE ILA ILIYO KOMONI NI MBILI
1 Whte- Inapendwa sana na wabongo kisa ni myeupe
2,Brown- Inapendwa sana na wazungu na wabongo wa chache, hii brown ina vitamini vyote make inatengenezwa na ngano ambayo haijakobolewa kuondolewa maganda

MKUU ILA KUTOKANA NA COMPETTION UNAWEZA AMUA KWENDA KUANZISHA HII BAISHARA KATIKA MIKOA MINGINE AMBAYO BADO HAIJAWA NA VIWANDA VINGI,

HATA WAWEKEZAJI WANO KUJA TANZANIA WANAKIMBIA COMPETITION HUKO KWAO

l
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…