Nataka kujifunza kupika chapati tamu

Nataka kujifunza kupika chapati tamu

jf user

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2018
Posts
777
Reaction score
623
Za kazi wakuu.
Napenda sana vyakula vitamu ila sijui kupika.
Leo nataka nianza na chapatti flani amazing, Hizi chapatti zinakua ni laini, nene, zina rangi nzuri ya brown kutokana na zimepikwa kiutaalamu. Ukila moja una shiba au maximum mbili.

Unaweza kula hizo chapatti na supu ya kuku, mchuzi wa maharagwe ya tui la Nazi, chai nzito ya maziwa, supu ya kongoro n.k
Naomben abc za kuandaa hasa kukanda unga kwani pale ndio inanitia shida pia kupaka mafuta mara kadhaa na kusokota tena huwa sielewi.


Chapati.jpg
 
Hakikisha kuna balance Kati unga na maji wakati wa kukanda
Pia weka chumvi moderate isiwe Kali Sana Wala chache,, wengine hupendelea kuweka na sukar kidogo

pia weka mafuta kidogo wakati unakanda ukishakanda acha uo mchanganyiko robo saa huku Ukiwa umefunika na karatasi Safi ili kuleta joto

Unamega Sasa vipande vyako kwa ajili ya kusukuma Mara ya kwanza. Ukubwa utategemea na Wewe mwenyew unavyotaka size ya chapati yako iwe

Ukishagawanya kwenye madunguli madogo madogo unaanza sukuma. Ukisukuma unapaka mafuta kiasi kisha unaviringisha Kama ngata. Ili mafuta yakolee Vizuri. Fanya hivyo kwa madunguli yote

Kisha unaanza sukuma izo ngata uzofunga tayari kwa kupika Sasa.

Rangi nzuri ya chapati zako utategemea na namna unabalance moto wako wakati wa kuipika
Kumbuka kuweka moto moderate.. Moto usiwe mkali Sana Wala hafifu Sana.
 
Back
Top Bottom