Hakikisha kuna balance Kati unga na maji wakati wa kukanda
Pia weka chumvi moderate isiwe Kali Sana Wala chache,, wengine hupendelea kuweka na sukar kidogo
pia weka mafuta kidogo wakati unakanda ukishakanda acha uo mchanganyiko robo saa huku Ukiwa umefunika na karatasi Safi ili kuleta joto
Unamega Sasa vipande vyako kwa ajili ya kusukuma Mara ya kwanza. Ukubwa utategemea na Wewe mwenyew unavyotaka size ya chapati yako iwe
Ukishagawanya kwenye madunguli madogo madogo unaanza sukuma. Ukisukuma unapaka mafuta kiasi kisha unaviringisha Kama ngata. Ili mafuta yakolee Vizuri. Fanya hivyo kwa madunguli yote
Kisha unaanza sukuma izo ngata uzofunga tayari kwa kupika Sasa.
Rangi nzuri ya chapati zako utategemea na namna unabalance moto wako wakati wa kuipika
Kumbuka kuweka moto moderate.. Moto usiwe mkali Sana Wala hafifu Sana.