Nataka kukopa kwenye benki ya kilimo ADB: Naomba wanaojua wanipe ushauri nifanyaje

Semlingwa

Member
Joined
Oct 21, 2018
Posts
7
Reaction score
5
Ndugu zangu humu jf nnajua humu kuna watu wa aina tofauti maboss wa mawizara na mabenk naomba muongozo wenu Mimi nikijana nimemaliza chuo tangu 2011,kwa kweli tangu nimemaliza chuo sijawahi kupata kazi ya maana ya kuweza kuniwezesha kujitegemea maana kama mnavyojua kazi za mauzo mtaani vitu vya promotion kitu cha elf 3 uuze 3500 ndio 500 yako unaweza kuzunguka kutwa mzima nikaambulia elf 5000 halafu hata Siku 2 nisipate kitu,Leo nimekaa nimefikiria nimeona nirudi kijijini nikafanye kilimo nimeamua kwenda kijijini sababu tunaeneo kubwa ambalo itakuwa rahisi kwahyo kama kuna anaye jua mashart ya kupewa mkopo maana mzee magu kila siku anatangaza kuna hela benki ya kilimo lakini sijui mashart yake nifanyaje maana nnajua itakuwa dsm hyo benk naweza kuja dsm nikakosa vigezo naomba mwenye uelewa vitu vinavyoitajika.
 
Kwanza nakupa hongera kama wewe kijana kwa kejua kwamba Ni vizuri kuweza kujishughueisha na kilimo hasa kilimo biashara,afu uzuri Ni kuwa kwa Sasa serikali inaompango mkakati{strategic plan} za kuwawezesha vijana moja kwa moja kwa kuwapa mikopo/mitaji ya masharti nafuu kwa kupitia taasisi mbalimbali Kama vile mabenki.
Ko miongoni mwa masharti nafuu yakukuwezesha kuweza kupata mkopo Ni;
•kuwa na collateral securities {hazina isiyo hamishika}Kama vile kiwanja au nyumba ko naona kabisa hapa umefit kwasababu umesema mnalo eneo kubwa la shamba ko unaweza ukaweka kidogo kwa makubaliano maalumu.
•Kuwa na business plan {wazo biashara} ambayo ndiyo inakuwa first mile yako kuelekea aina ya kilimo ambacho unataka kufanya hasa kilimo biashara kama kilimo cha mihogo,chai,korosho,ufuta,pamba,kahawa,ndizi,mchele,ufuta,alizeti,au hata kilimo cha matunda biashara kama tikiti maji pamoja na mizabibu.
•referees{wazamini}ambao watasimama Kama watu ambao wanathibitisha kwamba unao uwezo wakuweza kurudisha hizo pesa na pindi utakaposhindwa kuzirudisha wao watakuripia au kuwajibika kwa namna yeyote hile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…