Nafikiri unaweza as a concerned/affected individual and u have evidence. Disaini ya Mtikila style, au sijakuelewa?
Kimsingi unaweza kabisa kumfungulia mtu yeyoote yule mashitaka nchini Tanzania.
Jambo la msingi ni kuhakikisha kuwa hicho unachomshitakia kina public interests (malahi ya Umma). Kwa mfano mtu anachafua mazingira, mtu anaiba mali ya umma, mtu hatimizi wajibu wake aliopewa kisheria(kwa mfano Waziri wa Mambo ya ndani anweza kushitakiwa kwa kushindwa kuwalinda raia kama vile ile issue ya Albino).
Ukitizama Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 (kama ilivyofanyiwa marekebisho mara kwa mara) katika Ibara ya 27 inasema hivi;(nanukuu).....
(1) Kila mtu ana wajibu wa kulinda maliasilia ya Jamhuri ya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia kuiheshimu mali ya mtu mwingine.
(2) Watu wote watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya Mamlaka ya Nchi na ya pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhilifu, na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao. (mwisho wa kunukuu)
Kwa hiyo kama inavyobainishwa na Katiba ya Nchi yetu ni wazi kuwa ni jukumu la kila mwananchi kulinda na kudumisha mali ya Umma wa Watanzania. Kimsingi na kwa mujibu wa sheria hii mama,kila Mtanzania anayo mamlaka ya kufungua kesi katika mahakama yenye uwezo wa kisheria ili mradi tu dhana kuu ya kesi hiyo iwe ni kulinda maslahi ya Umma (for the public Interests).
Kesi za namna hii ndizo kama zile ambazo Mheshimiwa Mtikila amekuwa akizifungua dhidi ya Serikali tangu miaka ya tisini.(naungana na Kaniki) Hili linadhihirisha kuwa inawezekana. Hivyo naomba kutofautiana na Kang.