Uchaguzi 2020 Nataka kumpigia kura Mheshimiwa Rais Magufuli

Uchaguzi 2020 Nataka kumpigia kura Mheshimiwa Rais Magufuli

Luthertz

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2018
Posts
206
Reaction score
830
Ninataka kumpigia kura mheshimiwa Rias wetu. Lakini, nahitaji majibu ya kina kwa haya maswali yangu;

1. Miili ya ndugu zetu iliyokuwa ikiokotwa ufukweni mwa bahari. Ili jambo ni jipya. Watanzania hatukuwahi kuona wenzetu wakiuawa kama kuku. Hawa watu walikosa nini mpaka kuondolewa haki yao ya kuishi? Serikali yake haikukerwa na jambo ili.

2. Kwanini alikiuka katiba ambayo ameapa kuitunza na kuilinda? Kuzuia mikutano ya siasa kwa vyama vya siasa isipokuwa chama chake tu cha CCM, ni kuisigina katiba. Why did he bend the law?

3. Watanzania wenzetu waliotekwa na kupotezwa kwa kuwa tu mawazo yao yalikuwa tofauti na yake. Hapa ananipa majibu gani?

4. Serikali zenye viongozi waliostaarabika utambua uhuru wa all three arms of governments; legislative, judiciary, and executive. Huyu wetu kafanya mahakama zetu kuwa kangaroo courts, Bunge limekuwa moja ya jumuiya za CCM. Kwanini?

5. Nina maswali mengi ila kwanza tuanze na haya.
 

Safari hii hawana namna, itawabidi tu wategemee nguvu ya wale wasanii wao 100 na pia vitisho ili kuwavuta wananchi kuhudhuria mikutano yao ya kampeni.

Kwa akili zao wanadhani maendeleo ni kununua tu ndege na kujenga flyovers, huku wananchi wakitaabika kwa kuishi maisha magumu.
 
Back
Top Bottom