Nataka kununua gari aina ya Pajero i0, msaada kwa anayelijua

Nataka kununua gari aina ya Pajero i0, msaada kwa anayelijua

Everyday

Member
Joined
May 6, 2014
Posts
11
Reaction score
2
Wapendwa wana JF.
Nina nia thabiti na mapenzi ya kununua Pajero i0 na nimetokeo kupenda sana aina hii ya gari.
Nakuombeni sana wana JF kama kuna mwenyewe welewa juu ya gari hili ikiwa ni pamoja na matumizi yake ua mafuta
anijuze. Naomba kuwasilisha.
 
Mimi nijuavyo mimi Pajero ni vimeo zinasumbua sana kaka nakusihi acha kabisa unless uwe na mtu ambaye aliwahi kutumia gari ya aina hiyo na akakuhakikishia kwamba ni nzuri. Asilimia 90 ya watu wanaonunua Pajero ni Gerage kila siku na kulalamika.
 
Kwa pajero hapana kwani umeweka bajeti ya kiasi gani? ili nikushauri vizuri
 
kama ni mara yako ya kwanza kununua gari nakushauri usinunue mitsubishi pajero ni gari isiyovumilia mashimo ya lami zetu za kuunga,pats zake ni ghali e.g shock up,suspension ruber,coil springs
 
Gearbox yake itakusumbua. GDI engine yake ni nzuri ikiwa mpya ikila km nyingi utaweka gari juu ya mawe. Walionazo ni ushahidi tosha.
 
Wapendwa wana JF.
Nina nia thabiti na mapenzi ya kununua Pajero i0 na nimetokeo kupenda sana aina hii ya gari.
Nakuombeni sana wana JF kama kuna mwenyewe welewa juu ya gari hili ikiwa ni pamoja na matumizi yake ua mafuta
anijuze. Naomba kuwasilisha.

Hiyo nzuri ikiwa mpya, na baada ya miaka mitano utapata ugonjwa wa moyo kama afya yako ni ya kuungaunga. Bora hada gari dogo lenye uhakika na uimara litakufaa zaidi kuliko gari lenye jina kubwa lakini si imara na parts ghali hali kadhalika gari hiyo matumizi ya mafuta ni juu sana. Nimeipenda sana Suzuki Swift 4 wheel drive, inapenya milima, inapasua tope na majini inavuka bila shida, mchangani haikwami, ni nyepesi. Mafuta ni kunusa tu, hiyo nimepata uzoefu kwa kuitumia kwa wanaopanga bajeti vizuri ni mpango mzuri wa kubana matumizi.
 
Kaka achana nayo jirani zangu 2 walikuwa nazo kama hiyo hiyo ilikuwa ni majanga na kuuza pia ilikuwa ni shughuli kwani wengi walishazijua!
 
Wapendwa wana JF.
Nina nia thabiti na mapenzi ya kununua Pajero i0 na nimetokeo kupenda sana aina hii ya gari.
Nakuombeni sana wana JF kama kuna mwenyewe welewa juu ya gari hili ikiwa ni pamoja na matumizi yake ua mafuta
anijuze. Naomba kuwasilisha.
Ukinunua hiyo ni sawa na kufunga ndoa ya kikristo mbaka ije ikufie. Ata ukiwa na shida ya haraka dharura ukataka kuweka bondi haiuziki ukicompare na gari za toyota IST, Spacio au Rav 4.
 
Back
Top Bottom