Nataka kuolewa, ila nataka nieendelee na uhuru wangu

Makonde plateu

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2022
Posts
1,443
Reaction score
3,480
Ntaka niolewe lakini niendelee kuwa na uhuru wangu!

Nina mchumba wangu ambaye Mungu akipenda, mwezi huu mwishoni tunafunga ndoa. Hata hivyo, nimeshaanza kuogopa. Sio kwamba ananifanyia kitu kibaya au ni mtu mbaya, hapana, lakini kuna mambo yanatokea ambayo sijayapendi. Mchumba wangu ni daktari, anafanya kazi huko Shinyanga wilaya moja ya vijijini sana. Nilishafika huko, na kwa kweli ni sehemu ambayo siwezi kuishi kwa sababu nina maisha yangu Dar es Salaam, na marafiki zangu wengi wako huku.

Mimi ninafanya biashara, nina duka la vipodozi. Ingawa si kubwa sana, ndio linaanza, na ninaamini kuwa mbele ya safari litakuwa kubwa sana. Sasa juzi, wakati nikizungumza na mama yangu, aliniambia kwamba nikishaolewa nimwachie mdogo wangu hili duka, kwani siwezi kulisimamia nikiwa Shinyanga. Nikamuambai sshinyanga gani hiyo nani kakuambia anaenda kuishi huko aliniambia: "Unafikiri utaolewa ubaki Dar es Salaam?"

Nilimwambia mama kuwa nimeshaongea na mchumba wangu, na tumepanga nitabaki Dar, naye atahamishiwa huku. Mama alikaa kimya, na hicho kitu kilinikuna kidogo. Nikaamua kuongea na mchumba wangu na kumuuliza, "Je, unajua hatujaongea chochote kuhusu sehemu ya kuishi?" Alionekana kushangaa na kuniambia kwamba, "Si Tunakwenda Shinyanga."

Nilishtuka na kumwambia, "Mimi siwezi kuishi kijijini huko. Kwa nini usitafute uhamisho?" Akasema, "Uhamisho ni mgumu kupata, na isitoshe, sasa hivi mimi nakaimu Mganga Mkuu, nafanay mchongo ili niwe mkuu wa idara kamili. Nikihamia Dar, nitakuwa Mganga wa kawaida tu, na sipendi hilo."

Tuliendelea kugombana. Nilimwambia kuwa siwezi kuondoka mbali na Dar kwa sababu nina marafiki zangu, maisha yangu, na mipango yangu. Yeye akasema, "Siwezi kuoa mke ambaye anaishi mbali nami. Kama ni biashara, unaweza kuhamishia shinyanga."

Tumegombana, na kila mtu anaona upande wake ni sahihi. Mimi nahisi hii ndoa siwezi kuimudu. Kama mwanaume hajaniaoa tayari na anaanza kunipangia maisha, unafikiri itakuwaje nikishaolewa?

Mimi siwezi maisha ya kuendeshwa na mtu, natamani kuahirisha kila kitu kwa sababu siwezi kupangiwa maisha na mtu kisa ndoa. Naomba ushauri wako. Nikiwa hapa nyumbani hakuna anayenielewa, sasa sijui nifanye nini. Sina tena hamu ya ndoa!
 
Bado una ubinti haupo ready kwa ndoa.
Rule no 1 ya ndoa , "ndoa haijui mwerevu" . Umeenda shinyanga ukapiga msasa biashara kule opportunity ni zp ??
Je hao marafiki unawataja kwa mipango yao ya maisha ww upo ???
Biashara hujui kuwa inakufa au kunawiri??
ila kwa mtazamo wa points zako mpe jamaa tu uhuru wake akapange maisha na mwingine , ww haupo tayari ila jua fika kuwa kumpata soul mate in this life mpate connection ni next to impossible .
Fanya biashara mwana all the best , huyo jembe muachilie akatafute bahati kwa mwingine.
 
Achana naye huyo utaendaje kuishi maporini wakati Daslamu ndio kuna kila kitu
1000017057.jpg
 
Ntaka niolewe lakini niendelee kuwa na uhuru wangu!

Nina mchumba wangu ambaye Mungu akipenda, mwezi huu mwishoni tunafunga ndoa. Hata hivyo, nimeshaanza kuogopa. Sio kwamba ananifanyia kitu kibaya au ni mtu mbaya, hapana, lakini kuna mambo yanatokea ambayo sijayapendi. Mchumba wangu ni daktari, anafanya kazi huko Shinyanga wilaya moja ya vijijini sana. Nilishafika huko, na kwa kweli ni sehemu ambayo siwezi kuishi kwa sababu nina maisha yangu Dar es Salaam, na marafiki zangu wengi wako huku.

Mimi ninafanya biashara, nina duka la vipodozi. Ingawa si kubwa sana, ndio linaanza, na ninaamini kuwa mbele ya safari litakuwa kubwa sana. Sasa juzi, wakati nikizungumza na mama yangu, aliniambia kwamba nikishaolewa nimwachie mdogo wangu hili duka, kwani siwezi kulisimamia nikiwa Shinyanga. Nikamuambai sshinyanga gani hiyo nani kakuambia anaenda kuishi huko aliniambia: "Unafikiri utaolewa ubaki Dar es Salaam?"

Nilimwambia mama kuwa nimeshaongea na mchumba wangu, na tumepanga nitabaki Dar, naye atahamishiwa huku. Mama alikaa kimya, na hicho kitu kilinikuna kidogo. Nikaamua kuongea na mchumba wangu na kumuuliza, "Je, unajua hatujaongea chochote kuhusu sehemu ya kuishi?" Alionekana kushangaa na kuniambia kwamba, "Si Tunakwenda Shinyanga."

Nilishtuka na kumwambia, "Mimi siwezi kuishi kijijini huko. Kwa nini usitafute uhamisho?" Akasema, "Uhamisho ni mgumu kupata, na isitoshe, sasa hivi mimi nakaimu Mganga Mkuu, nafanay mchongo ili niwe mkuu wa idara kamili. Nikihamia Dar, nitakuwa Mganga wa kawaida tu, na sipendi hilo."

Tuliendelea kugombana. Nilimwambia kuwa siwezi kuondoka mbali na Dar kwa sababu nina marafiki zangu, maisha yangu, na mipango yangu. Yeye akasema, "Siwezi kuoa mke ambaye anaishi mbali nami. Kama ni biashara, unaweza kuhamishia shinyanga."

Tumegombana, na kila mtu anaona upande wake ni sahihi. Mimi nahisi hii ndoa siwezi kuimudu. Kama mwanaume hajaniaoa tayari na anaanza kunipangia maisha, unafikiri itakuwaje nikishaolewa?

Mimi siwezi maisha ya kuendeshwa na mtu, natamani kuahirisha kila kitu kwa sababu siwezi kupangiwa maisha na mtu kisa ndoa. Naomba ushauri wako. Nikiwa hapa nyumbani hakuna anayenielewa, sasa sijui nifanye nini. Sina tena hamu ya ndoa!
Na ukienda huko kijijini mwaka tu ukirudi kila mtu anakushangaa umepauka na umezeeka dar taamuuu.
 
Nyie ndio mnaolewa halafu mnapanda kitandani na nguo.

Una marafiki zako Dar kwa hiyo huwezi kuwaacha ukaenda Shinyanga kisa ndoa.

Ndoa sio kwa Kila mwanamke. Wengine ni kugongwa kujazwa mimba kuzalishwa na maisha yanaendelea.

Fanya vile moyo wako akili utashi na nafsi yako vinaridhia
 
Back
Top Bottom