Nina masters yangu ya Logistics,nimeifanyia Canada,na First degree yangu ni ya Accounts nimeifanyia Australia,working Experience 3 Yrs now,nafikilia kurudi nyumbani nimechoka kukaa ukimbizini kwa mda mrefu na nimemiss jamaa zangu kwa mda mrefu.
Kabla sijarudi naomba mnipe hali ya upepo huko kunalipa au hakuna kitu nitulie zangu huku,na kama ni ajira niombe wapi ambapo wanalipa fresh zaidi.
kujiajiri hilo alinisumbui hata kidogo kwa sababu najua naweza kujiajili..maisha yangu yako kwenye mstari kidogo,na mtaji ni nao wa kutosha.hata hapa ninapofanya wanalipa pesa nzuri najua hata kwa bongo hawezi kufikia robo ya malipo ninayopata..shida najisikia stress na kama hatia vile..napenda kuishi na jamaa zangu kwa karibu zaidi.kuna kitu naona kama kimenza kupungua hasa kuwa mbali na wazazi wangu na jamaa zangu kwa mda mrefu.kila nikija nakaa week mbili au tatu nakuondoka.kaka yangu ,mdogo wangu napenda kuwa nao karibu sana.sioni kazi kama inanipa furaha ninayotoka..