Nataka kusajili NGO kwa ajili ya kuwasaidia wakulima, naomba kufahamishwa yafuatayo

2018

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2018
Posts
546
Reaction score
779
Salaam,

Nimepata wafadhili wa mradi wa kilimo, lengo kuu ni kusaidia wakulima wadogo waweze kujikwamua na kunufaika na kilimo chao.

Sasa nahitajika niwe na NGO ili wafadhili waweze kuleta miundo mbinu kwaajiri ya mradi huo.

Kitu pekee kilichobaki ni kusajili NGO yetu ili tuweze kufanya kazi pamoja na wafadhili hao, OMBI langu kwenu wanajamvi ni kunisaidia niweze kujua taratibu za kusajili NGO ili tuweze kuwezesha jambo hili kwa faida ya taifa zima.

Karibuni kwa michango na maoni.

609a21835e7749c7ea0185bb_PVeg3HqpNwOo34Jwln_F71qtL-Tg46kGrZqbq2Y92MqsIXUpGeiFd_4HlEpYm2bKyhwk9...jpg
Screenshot_20220427-180029.jpg
 
Sawa mkuu ngoja nijaribu hilo, nikiona giza ntakurudia kwa msaada zaidi
 
TARATIBU ZA USAJILI

Usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali unaofanyika chini ya sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Na. 24 ya mwaka 2002 umegawanywa katika ngazi nne kama ifuatavyo:

1.1 Ngazi ya Wilaya

1.2 Ngazi ya Mkoa

1.3 Ngazi ya Taifa

1.4 Ngazi ya Kimataifa

Msajili wa Mashirika ya kiserikali amepewa mamlaka chini ya kifungu cha 22(1) cha sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24, ya mwaka 2002 kuteua maafisa wa umma katika wilaya au mkoa kwa ajili ya kuwezesha usajili katika ngazi husika. Katika mfumo uliopo sasa maafisa wa umma wanaotajwa katika sheria ni Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya na Mkoa ambao kwa namna nyingine huitwa wasajili wasaidizi.

Kwa mujibu wa kifungu cha 12(1) cha sheria, maombi ya usajili yatawasilishwa na kikundi cha watu kwa Msajili kupitia fomu maalumu (NGO A Fomu Na. 1). Maneno “kikundi cha watu” yanahusisha kikundi cha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali. Hata hivyo, kanuni ya 3 ya kanuni za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali zilizofanyiwa marekebisho mwaka 2015 kupitia tangazo la serikali Na. 8 inaweka sharti la kikundi kuwa na watu/wanachama wasiopungua watano.

Kulingana na Kifungu cha 12(2) cha Sheria ya NGOs Na. 24/2002, Maombi ya usajili wa NGOs yanatakiwa kuwa na viambatanisho vifuatavyo:-

Katiba ya Shirika lisilo la Kiserikali (Nakala 3 zilizojaladiwa – Bound).

Maelezo binafsi (Wasifu) wa viongozi 3 (CV) na picha 2 kwa kila CV – (Mwenyekiti, Katibu na Mhazini, au wengineo kulingana na mahitaji ya Shirika)

Angalizo: kwa NGOs za Kimataifa – CV mbili ziwe za raia wa Tanzania.

Muhtasari wa kikao cha kuanzishwa kwa Shirika ukiambatanishwa na majina na saini za wanachama waanzilishi.

Fomu ya maombi ya usajili (NGO A Fomu No. 1) iliyojazwa na mwombaji/waombaji na kubandikwa ushuru wa stempu za shilingi 1,500/= au Dola za Kimarekani 2 kwa NGOs za Kimataifa.

Barua ya Utambulisho kutoka kwa Msajili Msaidizi (Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa, Halmashauri /Manispaa/Wilaya).

Maelezo yoyote au taarifa kama itakavyohitajiwa na Msajili.

2.0 ADA ZA USAJILI

a)Ngazi ya Wilaya–Shs 80,000/=b)Ngazi ya Mkoa–Shs 100,000/=c)Ngazi ya Taifa–Shs 115,000/=d)Ngazi ya Kimataifa–Dola za Kimarekani 350

Maombi yatumwe kwa;

Msajili wa NGOs,

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,

8 Barabara ya Kivukoni

S.L.P 3448

11486 DAR ES SALAAM.

Simu 213526/2137679/2123146

Tovuti -http//www.tnnc.go
 
Salaam,

Nimepata wafadhili wa mradi wa kilimo, lengo kuu ni kusaidia wakulima wadogo waweze kujikwamua na kunufaika na kilimo chao.

Sasa nahitajika niwe na NGO ili wafadhili waweze kuleta miundo mbinu kwaajiri ya mradi huo.

Kitu pekee kilichobaki ni kusajili NGO yetu ili tuweze kufanya kazi pamoja na wafadhili hao, OMBI langu kwenu wanajamvi ni kunisaidia niweze kujua taratibu za kusajili NGO ili tuweze kuwezesha jambo hili kwa faida ya taifa zima.

Karibuni kwa michango na maoniView attachment 2250705View attachment 2250706
Check PM

Sent from my SM-T555 using JamiiForums mobile app
 
Hii orodha nimetumiwa Ijumaa ya tarehe 03/06/2022 pale ofisi za mkoa ustawi.

Ni hivi vifuatavyo:-
-Katiba
-Orodha ya wanachama waanzilishi.
-Nakala ya vitambulisho vya NIDA au LESENI ya udereva kwa wote.
-Fomu no 1 au no 3 ya NGO.
-Detailed CV ya viongozi watatu wa juu wa NGO na passports zao.
-Chati ya uongozi wa Shirika.
-Pia utatakiwa ulipie ada ya usajiri 115000 inalipwa online.
-Stamp duty ya TRA ya thamani ya 6000.

Ukiingia kwenye hii website utapata maelekezo yote ya usajiri nis.jamii.go.tz
 
TARATIBU ZA USAJILI

Usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali unaofanyika chini ya sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Na. 24 ya mwaka 2002 umegawanywa katika ngazi nne kama ifuatavyo:

1.1 Ngazi ya Wilaya

1.2 Ngazi ya Mkoa

1.3 Ngazi ya Taifa

1.4 Ngazi ya Kimataifa

Msajili wa Mashirika ya kiserikali amepewa mamlaka chini ya kifungu cha 22(1) cha sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24, ya mwaka 2002 kuteua maafisa wa umma katika wilaya au mkoa kwa ajili ya kuwezesha usajili katika ngazi husika. Katika mfumo uliopo sasa maafisa wa umma wanaotajwa katika sheria ni Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya na Mkoa ambao kwa namna nyingine huitwa wasajili wasaidizi.

Kwa mujibu wa kifungu cha 12(1) cha sheria, maombi ya usajili yatawasilishwa na kikundi cha watu kwa Msajili kupitia fomu maalumu (NGO A Fomu Na. 1). Maneno “kikundi cha watu” yanahusisha kikundi cha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali. Hata hivyo, kanuni ya 3 ya kanuni za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali zilizofanyiwa marekebisho mwaka 2015 kupitia tangazo la serikali Na. 8 inaweka sharti la kikundi kuwa na watu/wanachama wasiopungua watano.

Kulingana na Kifungu cha 12(2) cha Sheria ya NGOs Na. 24/2002, Maombi ya usajili wa NGOs yanatakiwa kuwa na viambatanisho vifuatavyo:-

Katiba ya Shirika lisilo la Kiserikali (Nakala 3 zilizojaladiwa – Bound).

Maelezo binafsi (Wasifu) wa viongozi 3 (CV) na picha 2 kwa kila CV – (Mwenyekiti, Katibu na Mhazini, au wengineo kulingana na mahitaji ya Shirika)

Angalizo: kwa NGOs za Kimataifa – CV mbili ziwe za raia wa Tanzania.

Muhtasari wa kikao cha kuanzishwa kwa Shirika ukiambatanishwa na majina na saini za wanachama waanzilishi.

Fomu ya maombi ya usajili (NGO A Fomu No. 1) iliyojazwa na mwombaji/waombaji na kubandikwa ushuru wa stempu za shilingi 1,500/= au Dola za Kimarekani 2 kwa NGOs za Kimataifa.

Barua ya Utambulisho kutoka kwa Msajili Msaidizi (Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa, Halmashauri /Manispaa/Wilaya).

Maelezo yoyote au taarifa kama itakavyohitajiwa na Msajili.

2.0 ADA ZA USAJILI

a)Ngazi ya Wilaya–Shs 80,000/=b)Ngazi ya Mkoa–Shs 100,000/=c)Ngazi ya Taifa–Shs 115,000/=d)Ngazi ya Kimataifa–Dola za Kimarekani 350

Maombi yatumwe kwa;

Msajili wa NGOs,

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,

8 Barabara ya Kivukoni

S.L.P 3448

11486 DAR ES SALAAM.

Simu 213526/2137679/2123146

Tovuti -http//www.tnnc.go
Shukrani sana mkuu
 
Back
Top Bottom