Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Ngoja In Shaa Allah niingie Maktaba:
Uingereza ilikuwa ikitawala Tanganyika chini ya kifungu 76 na 77 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Kama mamlaka tawala Uingereza ilitarajiwa kuanzisha na kuendeleza maendeleo ya siasa, uchumi na ya kijamii ya Tanganyika hadi kufikia wakati ambao watu wake wangekuwa tayari kujitawala. Lakini Waingereza walifanya khiyana na hawakutimiza ahadi hiyo. Walijihusisha na kulinda maslahi yao wenyewe ya kikoloni na yale ya watu weupe wachache na wakaendelea kuwapuuza Waafrika waliokuwa wengi na wenye nchi.
Ili Waafrika waweze kuikabili hali hii ilikuwa muhimu wawe wamoja kupambana na ukoloni na kwa ajili hii mwaka wa 1929 wakaunda African Association kwa nia ya kuwaleta Waafrika pamoja. Katika waasisi hawa kutoka Gerezani walikuwa Kleist Sykes (Katibu Muasisi) na Ibrahim Hamisi wote wakiishi Kipata Street. Lakini harakati khasa zilipamba moto baada ya Vita Kuu ya Pili pale mwaka wa 1950 vijana walipoamua kupindua uongozi wa TAA ambao Rais alikuwa Mwalimu Thomas Plantan akiishi Mtaa wa Masasi Mission Kota na Katibu Clement Mtamila akiishi Kipata. Walioongoza mapinduzi haya walikuwa Abdul Sykes na Hamza Mwapachu. Katika uchaguzi uliofuatia baada ya mapinduzi haya pale Makao Makuu ya TAA New Street Dr. Vedasto Kyaruzi akachaguliwa Rais na Abdul Sykes Katibu.
Mwaka huo TAA ikaunda TAA Political Subcommittee ambayo wajumbe wake walikuwa Dr. Kyaruzi, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Steven Mhando, Mufti Sheikh Hassan bin Ameir na Said Chaurembo. Kamati hii hadidu zake za rejea ilikuwa kushughulika na mambo yote ya siasa ndani ya TAA. Kwa msaada wa Earle Seaton ambae alikuwa rafiki yake Abdul huyu alikuwa mwanasheria kutoka kisiwa cha Bermuda TAA walianza kufanya mawasiliano na UNO kwa nia ya kutaka UNO iharakishe kupitia Kamati ya Udhamini wa Makoloni mchakato ambao utawaweka Waafrika wa Tanganyika katika hali ya kupewa uhuru wao. Hii Political Subcommittee ikapeleka kwa Gavana Twinig mapendekezo yake ya hali ya siasa Tanganyika na jinsi wananchi wanavyotaka nchi yao itawaliwe kufikia kupewa uhuru wake mwaka wa 1963.
Lakini viongozi hawa wa TAA walikuwa wanajua kuwa haiwezekani kudai uhuru chini ya TAA na ili kudai uhuru ni lazima wawe na chama cha siasa. Mazungumzo ya fikra hii yalianza mwaka wa 1951 kufanyika baina ya Abdul Sykes na Chief Kidaha Mwakaia wa Siha ambae alikuwa mjumbe wa LEGCO ikitegemewa Chief Kidaha ataingia TAA atachaguliwa Rais na TANU itaundwa kwenye Mkutano wa Mwaka wa TAA. Haya mazungumzo hayakufanikiwa.
Ndipo Hamza Mwapachu akaja na fikra ya kwa Abdul Sykes ya TAA kumtia Nyerere katika uongozi wa TAA New Street hii ilikuwa 1952 Nyerere alipotoka masomoni Uskochi na akaja Pugu kama mwalimu wa shule. Hadi kufikia mwaka wa 1953 mipango hii ikawa imekamilika pale Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe walipokwenda kwa Hamza Mwapachu Nansio, Ukerewe Abdul akitaka kupata kauli yake ya mwisho kutoka kwa Mwapachu kuhusu kumuingiza Nyerere kwenye nafasi ya urais wa TAA. Mwapachu alithibitisha kauli yake na katika uchaguzi wa mwaka wa 1953 Ukumbi wa Arnautoglo Nyerere akagombea nafasi ya urais dhidi ya Abdul Sykes na Nyerere akashinda. Mwaka wa 1954 katika Mkutano wa Mwaka wa TAA wajumbe 17 wa mkutano ule wakaunda TANU kama Hamza Mwapachu na Abdul Sykes walivyopanga.
TANU ikatangaza kuwa wameunda chama hicho kwa madhumuni ya kudai uhuru wa Tanganyika kiongozi wa harakati hizo akiwa Julius Nyerere. Mwaka wa 1955 Nyerere akaenda UNO kuhutubia Baraza la Udhamini akidai uchaguzi wa kura moja mtu mmoja katika LEGCO Baraza la Kutunga Sheria. Mwaka wa 1957 Nyerere akafanya safari ya pili UNO. Mwaka wa 1958 serikali ikaamua ufanyike uchaguzi ambao wajumbe watachaguliwa kwa rangi zao - Wazungu, Waasia na Waafrika. Uchaguzi ukafanyika na TANU ikashinda viti vyote. Mwaka wa 1960 Tanganyika ikapata madaraka na 1961 uhuru kamili.