Nataka kuvunja mji na kuuza kila nilichonacho ili nifungue biashara

Nataka kuvunja mji na kuuza kila nilichonacho ili nifungue biashara

Michael Ngusa

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2014
Posts
1,637
Reaction score
463
Habari zenu!

Jamani mimi nina business idea, ambayo tayari nina kila kitu upande wa paperworks na marketing strategies, kwa maana kwamba nina uhakika kampuni itasimama. Shida ni kwamba sina mtaji, hivyo nikafikiria nimrudishe home kwanza mke wangu ambaye pia ni mjamzito,

Akajifungulie huko na kusubiri mambo yangu yakae sawa,. Plan yangu ni kuuza kila kitu cha ndani kwangu halafu nihamie tu kwenye single room bei chee, kisha niache na kazi ili nichukue mafao yangu baada ya miezi 3, nikijumlisha hizo pesa inatosha kununulia vifaa vya kazi na kurent ofisi mjini, mnanishaurije? niko Arusha.
 
Una uzoefu na biashara unayotaka kufungua?
^^
 
Upo sahihi kabisa endelea tu na plan hiyo. Ila tu usimrudishe mke na mtoto kwao, banana nao huko huko kwenye bei chee.
 
Shauriana na mkeo ili mambo yakigoma msilaumiane
 
Huna akili kabisa...mkeo akajifungue kwa tabu kisa bussines?Tafuta mkopo acha ujinga
 
Habari zenu!

Jamani mimi nina business idea, ambayo tayari nina kila kitu upande wa paperworks na marketing strategies, kwa maana kwamba nina uhakika kampuni itasimama. Shida ni kwamba sina mtaji, hivyo nikafikiria nimrudishe home kwanza mke wangu ambaye pia ni mjamzito, akajifungulie huko na kusubiri mambo yangu yakae sawa,. Plan yangu ni kuuza kila kitu cha ndani kwangu halafu nihamie tu kwenye single room bei chee, kisha niache na kazi ili nichukue mafao yangu baada ya miezi 3, nikijumlisha hizo pesa inatosha kununulia vifaa vya kazi na kurent ofisi mjini, mnanishaurije? niko Arusha.
Mkuu pamoja na kwamba hujasema unatamani kuwa na mtaji wa sh. ngapi ili kuanza hiyo biashara
naona umechukua maamuzi magumu mawili 1.kuuza ulichonacho na 2.kuacha kazi.
Ushauri wangu ni kwamba kama hujawahifanya biashara hiyo unayotaka kuifanya usijaribu lkn kama ulishafanya na umepungukiwa na mtaji na sasa unataka kuongeza mtaji hapo endelea,ila nigekushauri uanze na uamuzi mmojawapo au kuuza asset zako huku ukiendelea na kazi au uache kazi utumie mafao kama mtaji huku una back up ya asset endapo kuna jambo halitaenda sawa.
Ila kwa ushauri wangu usijaribu kufanya biashara ambayo hujawahi jaribu kwa kufanya maamuzi magumu namna hiyo
hayo maamuzi tunayafanyaga tukiwa na uhakika na biashara unayoifanya kwamba itarudisha.
 
Swali la kizushi tu; Hivi huyo mkeo unamrudisha kijijini ili kupunguza stress ya ujauzito wake kwako au ni kukupisha ufanye ufisadi wako asikusumbue?
Uja uzito wa mkeo na kutaka kuuza vyombo vya ndani ukakae uswazi wapi na wapi? Sema unataka kuhama mji ili umkimbie mkeo na mtoto ukajifiche kusikojulikana wala si mtaji.
Mbuyu haukuanza kama ulivyo bali ulianza tu ka mchicha vile. Leo, haung'olewi kwa jembe la mkono. Biashara haianzi kwa mtaji mkubwa bali kwa wazo kidogo tu lililo buniwa vizuri, likaanzwa vizuri na mwishowe likawa kuubwa.
Usimsumbue mkeo, tayari ana hitaji saana ushirika wako. Siku hizi, tumepewa ruhusa kwenda naye mpaka pale mlango wa labour (Leba) tusubiri atuletee kichanga chetu tukakilee na yeye mpaka kikue tukiwa pamoja si yeye akae kijiji nasi tusage kitaa. Hayo ni mawazo potofu.
 
Hao wake zenu ni sawa na mizigo ya nazi eeeh mnarudisha tu????

Anyway all the best

Natumaini umefanya maandalizi ya kukea mtoto (au na mtoto utamrudisha)
 
Jerry mwandishi wa habari pingu na bastola vyanini, pingu haziuzwi popote bongo bastola sawa waweza sema ulinzi wake haya risiti hana na imekutwa loaded.

Hapo ndipo kwenye utata, Inawezekana jamaa wanataka kumfanya victim kwa kisasi, lakini hilo swala la mtu kumiliki pingu inakuwaje? Ni yule mzee wa Bagamoyo alisema kuwa Muro anamiliki Bastola na Pingu (kwa mujibu wa Kova), na kweli walimkuta navyo hivyo na amekubali kuwa ni vyake, sasa bunduki ni sawa ila Pingu inakuwaje? Jamaa yupo kwenye utata ingawa jamii inaona kuwa ni kisasi[/QUOTE]

Tunajua akili safi huleta mafanikio katika kutafuta,unaweza kua sawa juu ya kuuza ulichonacho ili kikusaidie,ila kwa upande wa pili usimludishe mkeo nyumbani kwao ni makosa,bola hata ungepanga kumpeleka nyumbani kwenu na usikate mguu huko kwenda kumuona na kumtunza,naona wazi utaingia kwenye shida juu ya ndoa yako siku za usoni
 
Hapo ndipo kwenye utata, Inawezekana jamaa wanataka kumfanya victim kwa kisasi, lakini hilo swala la mtu kumiliki pingu inakuwaje? Ni yule mzee wa Bagamoyo alisema kuwa Muro anamiliki Bastola na Pingu (kwa mujibu wa Kova), na kweli walimkuta navyo hivyo na amekubali kuwa ni vyake, sasa bunduki ni sawa ila Pingu inakuwaje? Jamaa yupo kwenye utata ingawa jamii inaona kuwa ni kisasi

Tunajua akili safi huleta mafanikio katika kutafuta,unaweza kua sawa juu ya kuuza ulichonacho ili kikusaidie,ila kwa upande wa pili usimludishe mkeo nyumbani kwao ni makosa,bola hata ungepanga kumpeleka nyumbani kwenu na usikate mguu huko kwenda kumuona na kumtunza,naona wazi utaingia kwenye shida juu ya ndoa yako siku za usoni[/QUOTE]

ungeona pesa ni ya msingi zaidi,ungetafuta kwanza ndio uoe...ila sasa usimtese mtoto wa watu...kuwa mwanaume, kula kwa jasho
 
Swali la kizushi tu; Hivi huyo mkeo unamrudisha kijijini ili kupunguza stress ya ujauzito wake kwako au ni kukupisha ufanye ufisadi wako asikusumbue?
Uja uzito wa mkeo na kutaka kuuza vyombo vya ndani ukakae uswazi wapi na wapi? Sema unataka kuhama mji ili umkimbie mkeo na mtoto ukajifiche kusikojulikana wala si mtaji.
Mbuyu haukuanza kama ulivyo bali ulianza tu ka mchicha vile. Leo, haung'olewi kwa jembe la mkono. Biashara haianzi kwa mtaji mkubwa bali kwa wazo kidogo tu lililo buniwa vizuri, likaanzwa vizuri na mwishowe likawa kuubwa.
Usimsumbue mkeo, tayari ana hitaji saana ushirika wako. Siku hizi, tumepewa ruhusa kwenda naye mpaka pale mlango wa labour (Leba) tusubiri atuletee kichanga chetu tukakilee na yeye mpaka kikue tukiwa pamoja si yeye akae kijiji nasi tusage kitaa. Hayo ni mawazo potofu.

ushauri mzuri sana. anamfanya mke kama zigo bwana...
 
Back
Top Bottom