Nataka kuvunja mkataba wa mauziano kabla malipo hayajakamilika, Je naweza daiwa fidia?

Nataka kuvunja mkataba wa mauziano kabla malipo hayajakamilika, Je naweza daiwa fidia?

Gtt

Senior Member
Joined
Apr 22, 2017
Posts
128
Reaction score
123
Habari zenu wana jukwaa la sheria

Niende kwenye mada moja kwa moja mwezi mmoja wiki kadhaa zilizopita kuna mtu nilifanya nae makubaliano ya kununua biashara yangu kwa kiasi cha milioni 4 na tukaandikishana akanipa milioni mbili kwanza na nyingine angenipa trh 20 mwezi huu kisha nimuachie ile biashara. Ila sasa moyo wangu umegoma kuuza hii biashara yangu nataka nivunje huu mkataba na nimrudishie pesa yake, je anaweza kunishitaki na kudai fidia?

Tuliandikishana serikali za mtaa.

Asante sana.

Naweka barua ya makubaliano.
 
Mkataba huo hapo
20220311_090621.jpg
 
Habari zenu wana jukwaa la sheria
Niende kwenye mada moja kwa moja mwezi mmoja wiki kadhaa zilizopita kuna mtu nilifanya nae makubaliano ya kununua biashara yangu kwa kiasi cha milioni 4 na tukaandikishana akanipa milioni mbili kwanza na nyingine angenipa trh 20 mwezi huu kisha nimuachie ile biashara.Ila sasa moyo wangu umegoma kuuza hii biashara yangu nataka nivunje huu mkataba na nimrudishie pesa yake, je anaweza kunishitaki na kudai fidia? tuliandikishana serikali za mtaa.
Asante sana.
Naweka barua ya makubaliano.
Ukisikia ukorofi nd'o huo!!!
 
Itabidi wewe ndio uinunue upya hiyo biashara kwa Tsh milioni 4 nne taslimu.

Hivyo hesabu una hasara ya milioni 2😁
 
Mkuu sitaki ukorofi bali nataka nimrudishie pesa yake tu maana nimeghairi kuuza.
Wasiliana naye huyo mtu,
Mwambie kuna mgogoro umejiri kati yako wewe na ama mkeo au baba yako au yako (kwamba mmoja wao ni shareholder kwenye hiyo biashara),
Kuwa hajaridhia kuiuza hiyo biashara kwa Milioni 4, badala yake anataka milioni 7.

Sasa ili kwenda sawa na yeye, mmeafikiana kumrejeshea jamaa pesa yake taslimu Sh. Milioni 2,
Ili mtafute mteja mwingine wa milioni 7.

Na huyo jamaa mtafute mapema iwezekanavyo kabla haijakaribia tarehe 20.

Ili asije kwenda kuchukua mkopo sehemu ili akulipe wewe.
 
Asante kwa ushauri wako
 
Leta hiyo 2 mil nimpelekee mkuu. Mambo yenu yatakuwa freshi tu, mbona?

NB: Kumbuka kutuma na ya kutolea
 
Wasiliana naye huyo mtu,
Mwambie kuna mgogoro umejiri kati yako wewe na ama mkeo au baba yako au yako (kwamba mmoja wao ni shareholder kwenye hiyo biashara),
Kuwa hajaridhia kuiuza hiyo biashara kwa Milioni 4, badala yake anataka milioni 7.

Sasa ili kwenda sawa na yeye, mmeafikiana kumrejeshea jamaa pesa yake taslimu Sh. Milioni 2,
Ili mtafute mteja mwingine wa milioni 7.

Na huyo jamaa mtafute mapema iwezekanavyo kabla haijakaribia tarehe 20.

Ili asije kwenda kuchukua mkopo sehemu ili akulipe wewe.

Hiv unajua maana ya maandishi tena yenye kumbukumbu serikalini hapo aongee na uyo jamaa kistarabu akigoma ndio imekula kwake
 
Watu mnatia hasira sana, tamaa mbele kwanini ulitaka kuuza mwanzoni?

Umekaa na hela yake umetatua shida zako unataka kurudisha bila retention fee??

Mpe 2.5M mmalizane huo ni mkopo
 
Umepata mteja mwingine ambae atakupa pesa ndefu zaid, trh 20 sio mbali vulimia tu
 
Back
Top Bottom