Ukisikia ukorofi nd'o huo!!!Habari zenu wana jukwaa la sheria
Niende kwenye mada moja kwa moja mwezi mmoja wiki kadhaa zilizopita kuna mtu nilifanya nae makubaliano ya kununua biashara yangu kwa kiasi cha milioni 4 na tukaandikishana akanipa milioni mbili kwanza na nyingine angenipa trh 20 mwezi huu kisha nimuachie ile biashara.Ila sasa moyo wangu umegoma kuuza hii biashara yangu nataka nivunje huu mkataba na nimrudishie pesa yake, je anaweza kunishitaki na kudai fidia? tuliandikishana serikali za mtaa.
Asante sana.
Naweka barua ya makubaliano.
Wasiliana naye huyo mtu,Mkuu sitaki ukorofi bali nataka nimrudishie pesa yake tu maana nimeghairi kuuza.
Wasiliana naye huyo mtu,
Mwambie kuna mgogoro umejiri kati yako wewe na ama mkeo au baba yako au yako (kwamba mmoja wao ni shareholder kwenye hiyo biashara),
Kuwa hajaridhia kuiuza hiyo biashara kwa Milioni 4, badala yake anataka milioni 7.
Sasa ili kwenda sawa na yeye, mmeafikiana kumrejeshea jamaa pesa yake taslimu Sh. Milioni 2,
Ili mtafute mteja mwingine wa milioni 7.
Na huyo jamaa mtafute mapema iwezekanavyo kabla haijakaribia tarehe 20.
Ili asije kwenda kuchukua mkopo sehemu ili akulipe wewe.