Nataka kuvunja ndoa yangu; mme amezidi kwa dogo dogo

Status
Not open for further replies.
usiogope mama dai kilicho chako uishi kwa amani
na hao mahawara endelea kuleta data
wengine wana ndoa zao kama wameharibu yako na wewe waharibie
toa majina yao na no zao kama kawa
 
hawara mwenyewe ndo huyo,mimi asingenibabaisha kabisa.Mbilia kama kweli wewe ni mke wa ndoa kabisa.Usigombane na mahawara wa mmeo kabisa au hata mmeo,mimi ningewakomesha hata kwa tindikali.
 

mkuu kuna watu watakushauri wengine watakubeza lakini pia nakushauri kama wenzangu kuwa uende kwanza kwa Jaji mkuu umweleze ikishindikana basi tafuta mwanasheria akuongoze ili upate haki zako zote. once again pole sana.
 

Pole sana,inauma na kuumiza hii. Mungu na akutangulie ktk hali ulionayo, ongeza maombi kwa kufunga kwa Imani. Hakika Mungu anajua haki yako na dhuruma uipatayo kwa mumeo. Atatenda, kila laheri mbilia
 
Pole MBILIA, jambo la kwanza unalopaswa kufanya ni kupeleka suala lako kwenye bodi ya usuluhisihi wa ndoa (Marriage Conciliation Board). Hii ni kwa sababu kulingana na Sheria ya Ndoa Sura ya 29 kesi zote za talaka ni lazima zianzie kwenye bodi ya usuluhishi wa ndoa. Usipopeleka bodi mahakamani utawekewa pingamizi na kesi ya talaka itafutwa.( ila hutapaswa kupeleka suala lako bodi ikiwa kuna mazingira maalumu ya kukuzuia kwenda bodi mfano mumeo hapatikani nk). Bodi itajaribu kuwapatanisha na ikishindikana watatoa karatasi inayoonyesha kuwa wameshindwa kuwasuluhisha, hapo ndo utakuwa na uwezo wa kudai talaka mahakamani. Siku nyingine ukipigwa ni vyema ukaripoti polisi ili uwe na record kuwa ulishawahi kuteswa (kupigwa) na ulirepoti tukio hilo polisi. Huo utakuwa ni ushahidi kuwa ulikuwa wateswa (cruelty). Pia kusanya majina ya hao wanawake wengine wa mumeo pamoja na watoto wa nje ya ndoa wa mmeo, kama wapo na ushahidi kuwa wanamahusiano ili uweze kuthibitisha uzinzi wa mumeo. Kumbuka kutambua mali zote mlizozichuma wakati wa ndoa hata kama zipo kwa jina la mume tu, ili uweze kudai mgawanyo wa mali. Mwisho, ni vyema ukatafuta wakili ili akusimamie shauri lako.
 
Binafsi nawakilisha kilio cha wake za wanasheria duniani.Wengi wameuawa na kupigwa wakakosa hata pa kushitaki. Mfano tunao wa mama yule wa Mkwepu Posta. lakini ushahidi wote ulitupwa kwa kisingizio kuwa yule mtoto wao angekosa mtu wa kumlea. Hivyo for the first time maiti akakosa haki. Je, damu yake ilikuwa maji?

Nitapigania haki yangu hata kama nikifa. Sioni faida ya ndoa iwapo huko ndani mimi ni mtumwa.
 
Reactions: SG8
Mbilia nimepiga hizo namba hazipatikani! AMA zimezimwa?
 
MKA thanx very much. Hiyo bodi naendaje? Nipo dar. mali zote najua zilipo hata nyumba alizojengea mahawara najua zilipo.
 
Inawezekana pia ni mke halali wa huyo jaji. So just give her a benefit of a doubt for now. The truth will ultimately come out.
I was married on 27th April 1991 keko Lutherani Church at 16:30. We engaged in year 1988 At the UDSM. Aliyefunga ndoa yetu alikuwa Mzee malasusa (Baba ya..)
 
Atakuwa miongoni mwa majaji walio tajwa na Lisu
 
sielewi yafuatayo.

Mtu wa miaka 45+ kushindwa suluhisha ndoa yako kwa busara bila kuathiri maslahi ya familia. Eti wazazi hawapo, wakati huo huo unajiandaa kupata wakwe toka kwa watoto wako, utawasaidia kusuluhisha nini?

Kuweza muanika mmeo halali kwenye mitandao ya kijamii kama hii, kwa mtu wa miaka 45+ nashinda mwelewa.

Hii panic ya jana kaipata wapi maana ndoa ya miaka 21 tabia ya mmeo kama ya umalaya haijaanza jana tu, huo mshangao wa jana umetoka wapi??

Ukiachana na ushabiki, utafurahi ukiona mama yako kachukua njia hii kusuluhisha mgogoro wa ndoa, hata baba yako mkosaji??

Hajawavua nguo familia nzima? Labda mie nayechangia hapa ndio kijana wake wa chuo kikuu atajuaje??

Katika familia chunga hasira zako zisiathiri watu wako wa karibu, hivi ameshindwa hata shirikisha watoto wake kabla hajaweka details zote hapa??

Haya huyo jaji mahakama kuu ya ardhi si anajulikana, wabaya wake hata wa kazi hawatataumia hili against himu??

Hapo hapo usifikiri kaacha kuwa tegemezi kwa huyo mmewe, bado ni tegemezi kwa jinsi navyomuona.

Hakuna mwanamke mwenye upeo anaweza fanya hili kwa familia yake ni boya tu.
Hapa watu tunashabikia sababu tunataka umbea si kwamba tunaumia naye kivileee, ila kachemsha mbaya, hasa nikiangalia na umri wake.

Kitu gani humuelewi mkuu?
 


ninyi watu wawili mmeongea ujinga kama mna akili za kuku wa kisasa vile. nampongeza CHUAKACHARA, ameongea point na nafikiri mama akichukua hatua/ushauri huu utamsaidia. aende kwa jaji kiongozi etc kama alivyoshauriwa. lakini ninyi wengine wawili ambao nimewakoti hapa, akili zenu ni za kinyama sana. hamfai kutoa ushauri kwa mtu ambaye yuko kwenye tatizo, mnaweza hata kumshauri mtu anywe sumu ili afe. akili zenu ni za shetani kabisa. nasema hivi kwasababu ukisoma uyu mama alivyoongea, na thread zake mbili alizoanzisha, utakuta kuwa, pamoja na kwamba anaomba ushauri wa kutaka talaka, sio kwamba anataka talaka. bado anaonekana kumpenda mumewe na anahangaika kumpokonya kutoka katika mikono ya malaya hao aliowataja. kwenye thread yake moja ameongea kuwa amemuona mumewe anaongea na simu akahisi anaongea na mwanamke wake. nafikiri huyu mama ana mpenda sana sana mumewe ndo maana ana wivu wa aina hii. ana wivu sana sana. na amekasirika amefikia mbali sana, anahitaji msaada ili chochote atakachokifanya kwa sasa asijekujilaumu baadae kuwa alienda haraka. kwa kifupi ni kwamba, kama mnasema ukimwi, akiachika, huyu atakayeenda kumpata mpya wa kuzeeka naye atakuwa salama? atakuwa na upendo wa rohoni kuliko yule aliyekaa naye miaka 21? unajua kuwa mtu ukioana naye mkakaa miaka yote hiyo ni sawa tu na mwili mmoja? hatawakuja waachane kamwe hata kama watatengana na kutengana kwa aina hii huleta vidonda ndugu kwenye mioyo na mvurugano wa ajabu. siku ingine muwe na akili kushauri watu mambo mazuri, msiwatumbukike shimoni zaidi wakati mnaona wapo kwenye wakati mgumu. watakuja kuwalaumu hasira zao zikiisha kuwa mliwashauri vibaya. yaani hapa jf kuna watu wengine huwa naweza amini kuwa sio binadamu wa kawaida, labda majini nayo yametengeneza account humu ili kuharibu watu. akili za kishetani kabisa kutoa ushauri kama huo kwa mtu ambaye yuko njia panda.....kama ukimwi unaweza kuupata popote pale, na kama huna mume au mke kama nyie mliotoa ushauri huu ndo ukimwi utaupata haraka kuliko wengine. akitengana huyo atapata ngoma fasta kuliko akiwa kwenye ndoa yake ya 21 years. NINYI MLIO TOA USHAURI MBAYA, KAMA NDOA ZENU ZILIWASHINDA MSITAFUTE WANACHAMA WENZENU WA TALAKA, bakieni na matalaka yenu hukohuko...mnaongea kama vile ndoa ziliwashinda na mnataka kila mtu afuate nyayo zenu..mnakera sana aisee.
 

Usidhani jambo hili limeanza leo hata nipaniki. Since 199... Lakini ninaposema nimechoshwa. Siyo tu ninangeo bali mangeo ya miaka. Ukimwalika msuluhishi anamchukia mtu huyo. Sasa ana marafiki anwalaani kila siku kwa mimi kuomba suluhu toka kwao. Tabia hii sisi wazee tusipoisema vijana itawathili. Unakimbilia kwa watu kakufukuza na midamu tele kisha anawachukia wale watu.
 
Mimi sioni kama amemuanika hadharani mme wake, coz hajamtambulisha kwa jina na hata huyu mama I'm sure MBILIA ni jina la bandia tu! Kwa hiyo kilichotajwa hapa ni situational not personal inawahusu WAKWARE wote.
 
Kwa kweli muhishimiwa kachemka sana kama ni kweli, napenda nichukue nafasi hii kukupa pole sana mama muhishimiwa, najua uko kwenye wakati mgumu sana lakini itakubidi ujitahidi kuwa imara, watoto wanakutegemea sana maana hawa jamaa wakishatekwa huwa wanasahau mpaka watoto. Pole sana!

Kuna haya maneno amabayo kama sikosei yanatoka kwenye maandiko ya Mungu: "Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, na mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe."

Utafiti usio rasmi unaonyesha kuwa kwa kiwango fulani mwanandoa kutokuwa mwaminifu huchangiwa na tabia za mwenzake ambazo hazipalilii uhusiano wa ndoa. Tatizo letu huwa tunafikiria tunakoangukia badala ya kujiuliza tulipojikwaa na sababu zilizotufanya tujikwae.

Ushauri: Badala ya kufikiria kuibomoa nyumba yako jitaidi kufikiria jinsi ya kuijenga, na itakuwa vizuri kama utaomba ushauri wa kuimarisha nyumba yako badala ya kuomba ushauri wa kuivunja, najua JF iko na wataalam wengi watashauri na sisi wengine tutajifunza kupitia kwenye ushauri hasi utakaotolewa.
 

Mimi sioni kama amemuanika hadharani mme wake, coz hajamtambulisha kwa jina na hata huyu mama I'm sure MBILIA ni jina la bandia tu! Kwa hiyo kilichotajwa hapa ni situational not personal inawahusu WAKWARE wote.
 
wee ni msafi hivyo?

Huna waa hata moja?

Sijaelewa ulivyotumia neno kafiri, pagani na anayemjua Yesu kutokuwa human beings.

Hadhi gani? mtu ambaye ni kahaba au fisadi au mwizi au pagani i.e mtu asiyemtii Yesu au kafiri ana hadhi gani ya kuitwa human being?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…