Bunny Wailer
Member
- Oct 29, 2017
- 11
- 11
Habari wana jamvi...!!
Nina tatizo na ningeomba nipate ushauri wenu ikibidi muongozo wa namna gani nifanye ili kupata ufumbuzi na haki zangu. Ni hivi, miezi sita sasa nimepoteza ajira kwa kufukuzwa na mwajiri wangu. Baada ya kupoteza ajira, nilienda ofisi za watu wa ppf kufuatilia mafao yangu. Lakini walichonambia ni kwamba, wamesitisha utoaji mafao mpaka wapate maelekezo toka serikalini, hiyo ilikuwa mwezi wa tano. Nikajipa moyo nikiamini maelekezo ya serikalini yatatoka ili nipate mafao yangu kutoka ppf. Kwa kipindi ambacho nilikuwa nikisubiri maelekezo ya serikalini kwa watu wa ppf ambayo ndiyo yangekuwa kama tiketi ya mimi kupata mafao, nilikuwa kutafuta ajira huku na huko, ila kwa kweli ajira zimekuwa ngumu sana kupatikana. Miezi miwili baadaye nikaenda tena ppf kutaka kujua, na majibu yalikuwa yaleyale kwamba wanasubiri maelekezo toka serikalini. Lakini nilipodadisi sana kwa maswali, niliambiwa na yule mhudumu kuwa, mafao yanatolewa kwa waliopunguzwa makazini/redundancy. Nilipouliza kama wanatoa kwa waliopunguzwa kazini, iweje waliofukuzwa wasipewe, yule mhudumu alinijibu vizuri kabisa kuwa maswali kama hayo hata wao huwa wanajiuliza na huwa hawapati majibu.
Wana jamvi, tangu kupoteza ajira nimekuwa na maisha ya shida sana, mambo yangu mengi yamevurugika, sina pa kushika, sina mjomba wala shangazi wa kunisaidia. Ninavyoishi Mungu pekee ndiye anajua. Nyumba niliyokuwa naishi ni ya kupanga, ilinibidi niondoke baada ya kodi kuisha. Nimekuwa naishi kwa kaka yangu ambaye nyumba yake nayo ilibomolewa huko Mbezi, hivyo naye anaishi kwenye nyumba ya mkwe wake. Mimi amenipa hifadhi kwa muda na hata hivyo nyumba yenyewe ya mkwe wake haijaisha kiujenzi kwa hiyo ninalala sebuleni. Kwa sababu nyumba ina vyumba viwili cha kwake na mkewe na kimoja cha watoto wake wawili wa kike ambao ni wakubwa.
Wana jamvi, lengo langu lilikuwa nifanye biashara yangu mwenyewe kwa hela hiyo ya ppf, lakini imeshindikana kwa sababu pesa yangu imezuiwa na hawa ppf kwa maelezo kuwa wanasubiri maelekezo toka serikalini. Kaka yangu mwenyewe hali yake kiuchumu si nzuri, kwa hiyo si rahisi kunipa mtaji. Kutokana na kuwaeleza watu tatizo langu, kuna mtu amenishauri niende mahakamani kuwashitaki ppf ili wanipe mafao yangu. Mtu huyo amenambia, msingi wa kesi yangu upo kwenye 'ubaguzi' kwamba; ppf wanatoa mafao kwa watu waliopunguzwa kazini ila wanabagua waliofukuzwa kazini, ilihali hakuna sheria ya namna hiyo. Amenieleza kuwa, hakuna sheria inayosema kuwa waliopunguzwa/redundancy watapewa mafao na ambao wamefukuzwa hawatapewa mafao. Sasa shida yangu ni moja hapa, kama naenda mahakamani hela yangu yenyewe ni hiyo milioni mbili na kama laki mbili, je, mwanasheria nitamlipa nini?
Naombeni ushauri ndugu zangu.