Nataka kuwashitaki PPF, naombeni mawazo na muongozo mzuri.

Mkuu tafuta vizuri data PPF wanalipa fao la kujitoa ila kwa conditions fulan fulan kama Redundancy na project kuisha ila sio kufukuzwa au kuacha kazi
 

Sasa angalia, wewe unazungumzia gari la kampuni, laptop ya kampuni kwamba kampuni inaku-provaidia, hayo uliyoyataja kwa wengine ni anasa kabisa. Usi-mention laptop ndugu. Kuna watu wanalipwa mishahara ukisikia utaogopa, mtu analipwa elfu 80 ambayo hiyo kwa mwingine ni pocket money ya mtoto wake. Tunatofautiana sana, ndiyo maana nikasema tuangalie aina ya maoni, mazingira kabla hatujachangia. Asante lakini maana nilitegemea ungerudi na hasira kama mbogo.
 
Asante ndugu kwa hilo. Maana kuna nyakati mtu analeta mizaha wakati si nyakati za mzaha.
 
Kati ya sheria mbovu kabisa nchi hii ni hizi sheria za mifuko ya hifadhi ya jamii. Hazijielew kabisa, zinazungumza masuala kama tupo mwaka 47 nakati zama zimebadilika kabisa. Zimekaa kama zinahudumua watumishi wa umma tu
 
FAO la kujitoa PPF lilikuwepo,waliliondoa tu mkuu.
 
Bunny Wailer kabla hujafungua kesi nenda SSRA ukajaribu kupata ufafanuzi kwanza
Asante Belo. Ni moja ya ushauri ambao pia nimepata toka kwa baadhi ya watu kwamba niende kupeleka malalamiko yangu huko SSRA, yasiponiridhisha ndipo niende mahakamani. Asante tena.
 
Asante Belo. Ni moja ya ushauri ambao pia nimepata toka kwa baadhi ya watu kwamba niende kupeleka malalamiko yangu huko SSRA, yasiponiridhisha ndipo niende mahakamani. Asante tena.
Kiongozi SSRA hawana msaada wowote. Nenda lakini utakuja kunipa mrejesho.

Hakuna kitu cha maana watakachokuambia.
 
Kiongozi SSRA hawana msaada wowote. Nenda lakini utakuja kunipa mrejesho.

Hakuna kitu cha maana watakachokuambia.

Kuna mchangiaji mmoja nilivyomuelewa, alitoa ushauri huo wa kufika pia SSRA ili majibu yao yatumike kama reference wakati wa kufungua kesi. Kwa hiyo bado ni muhimu, kwa sababu mwisho wa siku ikitokea mlalamikaji amefika mahakamani, na ikaonesha kuwa hajafika SSRA inaweza kusumbua. Kwa hiyo kutembelea SSRA ni muhimu si kwa sababu ya kupata msaada toka kwao ila kwa kukamilisha taratibu ama hatua za kufungua kesi, kwa hiyo ni lazima na muhimu kwenda huko kwa hao SSRA.
 
Cha The GREAT, sina pingamizi kwenda SSRA. Natamani aende hata kesho ili atupe mrejesho.
 
Hilo ndiyo jibu!
 
PPF hawashitakiwa chukua maji umezee utapona maumivu ya kichwa
 
Sitaki hata kuangalia herufi hizo PPF maana wanyanyasaji sana. Unapounganishwa nao hakuna Maelezo yoyote lakini ajira ikikoma utaambiwa hata umri wako
 
64gb FAO LA KUFUKUZWA KAZI HALINA UHUSIANO NA FAO LA KUJITOA (WITHDRAW)

PIA, SUALA LA KUREJESHEWA MICHANGO BAADA YA KUACHISHWA KAZI HALIANGALII SERA YA MFUKO, YANI NA LAZIMA UREJESHE HYO MICHANGO KWA SABABU NI SEHEMU TERMINAL BENEFITS KWA MTU ALIYEACHSHWA KAZI.
 
😵😵😵 mkuu fuatilia vizuriiii haya mambo wanakosea watu wa mifuko huwa hawatoi elimu nzuri kabla ya mwanachama kujiunga. Hakunaga FAO LA KUFUKUZWA KAZI kwenye social security, labda uniambie unemployment benefit ambayo Tanzania bado hakuna mfuko unaotoa. Kumbuka social security schemes siyo kama bank unaweka pesa ukiitaka unatoa, ndo maana mifuko ililazimishwa itoke kwenye provident funds kuja kwenye pensions fund. Target kubwa ni kumfanya aje awe mfaidika hadi uzeeni sasa ukifukuzwa kazi haimaanishi utashindwa kuchangia kwenye mfuko wa jamii, zaid zaid watakutoa kwenye mandatory scheme na kukupeleka kwenye voluntary scheme mfano wote scheme kwa PPF ambao hauna limitations kwenye uchangiaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…