Nataka kuwashitaki TRA kwa unyanyasi wa kodi ya barabara

Prof Decentman

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2013
Posts
276
Reaction score
140
Nimechoka kuishi kama digidigi ktk nchi yangu mwenyewe. Siku zote TRA walikuwa wapi kutoa elimu juu ya road licence? Kwa nn mnakamata gari lililo na vibali vyote ili kulipia gari ambalo halitembei??

Naomba ushauri wa kisheria kuwashitaki TRA kwa kutotimiza wajibu wao kutoa elimu hii ya kodi na pia kunisababishia usumbufu na kuishi kwa hofu. Pia wanilipe fidia kwa madhara niliyoyapata.

Kama kuna mwanasheria au yeyote anayeweza kunisaidia kuweka hoja zangu sawa anisaidia.

Pia kama kuna walioathirika na vitendo hivi tuungane kutetea haki zetu.

Kimsingi hatukatai kulipa kodi lakini kwa kuwa uzembe ni wa mamlaka ya kodi wanapaswa ku-face consequences kama tunazokabiliana nazo sisi.

Karibuni kwa michango.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…