kuna jamaa wanaitwa umeme jua wako hapo ubungo milenium business park (karibu na kiwanda cha urafiki au mataa ya shekilango) waone kesho utapata jibu zuri. Nadhani wao gharama zao ni chini ukilinganisha na Rex. rex walinifungia umeme wa taa 6, TV na Radio miaka kama 5 iliyopita nilitozwa kama 2m na usafiri mpaka kijijini ulikuwa wangu. Kibaya ni kuwa system haijatengemaa mpaka leo. Kila nikiwambia wakawa wananiyeyusha mpaka warrant period ikaisha. Wakaniambia ninunue bettary nyingine nikabadirishe, nayo haikusaidia. Sasa hivi hakuna cha TV wala radio, ni taa tu. tena mtu akijifanya kuchaji simu muda mrefu, usiku mnalala giza. Kwa kweli customer care yao sikuipenda ndio maana nawachukia mpaka leo