Nataka kwenda vitani kujitolea kuisadia Ukraine πŸ‡ΊπŸ‡¦, je nifuate utaratibu gani?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Nikiwa kama mkazi wa sayari hii tuliyo rehemishwa na Mwenyezi Mungu tuikalie kwa haki, amani na usawa, nina laani uvamizi wa Russia πŸ‡·πŸ‡Ί nchini Ukraine πŸ‡ΊπŸ‡¦.

Siishii tu kulaani na kukemea uvamizi huo, bali kwa hiari yangu na ridhaa ya familia yangu, tukiwa kama watetezi wa wanyonge, wanaoonewa, familia yangu imenituma niende mstari wa mbele wa mapambano, nikashike bunduki kumuondoa Mrusi ndani ya mipaka ya ardhi ya Ukraine πŸ‡ΊπŸ‡¦ aliyoiingia kimabavu.

Ndugu wana JamiiForums, naomba mine muongozo wa namna gani nitaweza kuyafikia malengo ya familia yangu ya kuwa askari wa hilarious wa Ukraine πŸ‡ΊπŸ‡¦.

Natanguliza shukrani za dhati.
 
Mapambano ya ndani dhidi ya mafisadi na wabugia keki ya taifa peke yao sio mapambano dhidi ya wanyonge ?

Au wewe ndio wale wachache waonea wengi kwahio hivi vita vya ndani havikuhusu....
 

Heri wewe mkuu kuliko wale mburumundu wanaoshabikia vita kana kwamba yanayoendelea ni mazuri, wanaokufa ni halali yao wakiwamo wanawake na watoto.

Afanyaye cha aina ya alichokifanya Putin, awe ni Bush, Amini au yule wa Ethiopia mtu huyo ni mwovu wala si pungufu ya hapo anachostahili si pongezi bali kutiwa adabu vilivyo.

Putin anastahili kukabiliwa si kuchekewa.
 
Kweli kabisa, Putin asichekewe.
Kumkalia kimya ni janga kwa dunia
 
Unipitie hapa Sinza mori
 
mpigie simu abubakar shekau wa bokoharam, anaijua njia vizuri atakuelekeza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…