Nataka niache kazi, nitafute goli Kariakoo niendeleze biashara hii hii ya nguo

Gap kibiashara lipo kwakweli
Drop job fill the gape. Ila mimi Sina Iman kubwa na Hilo... Otherwise biashara iweze kukulipa mshahara zaidi ya kazi yako na faida ibaki paleple. Usije ukaileta deni la kujilipa Kwa kukata faida uliyokuwa unaipata
 
Nafikiri kabla ya kuacha kazi umeshaweka suala la mtaji wa hiyo biashara sawa, kama ni hivyo fanya hivi tafuta hela ya kumkatia bima ya mwaka mzima au miaka miaka miwili mama yako anayeumwa najua katika kipindi cha mwaka au miaka miwili utakuwa umeshasimama kibiashara unaweza kumsaidia mama kwa kipindi cha miaka mingine miwili wakati huo huo biashara inaendelea kukua na kumarika. uwe na siku njema.
 
Asante sana kwa ushauri
 
Hakuna jambo lisilo na changamoto kila upande una faida na kila upande una hasara choose wisely
 
Mimi siamini katika kuajiriwa naamini kwenye kujiajiri, mimi mwenyewe nakushauri kama kibunda unacho kinachoweza kumudu kuanzisha biashara wee zama mzigoni cha kuzingatia hela ya bima ya mama iwepo.
 
Amka usingizi mdogo wangu.
Wewe inaonekana una kipaji cha biashara.

Trust me acha kazi fanya biashara yako suala la bima hata wewe mwenyewe unaweza kumlipia mama yako.
Hofu imewafanya watu wengi washindwe kufikia ndoto zao.
Unaweza unaweza.
 
Kama shida yako ni suala la bima ya mama bhasi hilo utaweza solve kiurahisi mbona acha kazi pambana na vyako
 
Mimi siamini katika kuajiriwa naamini kwenye kujiajiri mimi mwenyewe nakushauri kama kibunda unacho kinacho weza kumudu kuanzisha biashara wee zama mzigoni cha kuzingatia hela ya bima ya mama iwepo.
Shukrani
 
Amka usingizi mdogo wangu.
Wewe inaonekana una kipaji cha biashara.

Trust me acha kazi fanya biashara yako suala la bima hata wewe mwenyewe unaweza kumlipia mama yako.
Hofu imewafanya watu wengi washindwe kufikia ndoto zao.
Unaweza unaweza.
Asante sana mkuu wacha nipambane
 
Pata goli kwanza Kkoo, start operation baada ya muda utaweza kuwa na ground nzuri ya decision yako na come up na conclusion ya kuacha kazi uendelee na bizness au u operate both!!
 
SimaMa vizuri kwenye biashara ndo uache kazi
Hawezi kusimama kwenye biashara kabla hajaacha kazi
Note hakuna mwanajeshi anaependa kwenda vitani hapa duniani ni kwasabab imebidi tu.
 
Pata goli kwanza Kkoo, start operation baada ya muda utaweza kuwa na ground nzuri ya decision yako na come up na conclusion ya kuacha kazi uendelee na bizness au u operate both!!
Catalyst ya kujiimarisha kibiashara inaletwa na hofu baada ya yeye kuacha kazi over
 
Acha kazi unaogopa nini nchi imefunguka pesa zimemwagika mtaani una uzoefu wa biashara hofu ya nini? au hutaki utajiri?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…