Nataka nianze kubet

Author

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2014
Posts
1,715
Reaction score
8,058
Habari wana JF

Binafsi nimepanga nianze kubet ila sina ufahamu wowote na huu mchezo...kwa wale wakongwe naombeni uzoefu...nataka nibet kwenye mpira wa miguu. Naomba kufahamu:

1.Ni kampuni ipi nzuri ya kubet, huwa naona Mbet, SportPesa, Premier betting n.k. ipi nzuri?
2.Jinsi ya kubet, ni njia ipi rahisi ya kupiga mpunga
3.mambo mengine muhimu ya kuzingatia kabla ya kubet
 
Nikiambiwa nijifunze kubeti au niende kufanya mtihani wa form four bila maandalizi nitaenda kufanya mtihani wa form four bila maandalizi.

Kubeti ni kugumu.
 
Siyo kuneti tuu wapelekee hiyo hela yako ambayo haina kazi wale jamaa wanaojiita aim globl au fofeva living... sijakosea hayo majina ni uandishi ruu
 
Jamaa kaacha kazi anabet team mbili kwa siku...tatizo no odds mkuu..odds 2 dau laki tano
 
faza utaliwa maana wanaume wote waliowahi kubet wameliwa huo ndo ubaya wa huo mchezo
 
ndugu fungua uzi wako, sidhani kama ni busara kuleta tangazo lako kwenye threads mbalimbali.
 
Dah,achana na mawazo hayo mkuu.

Mimi nilianza kubet miaka 4 iliyopita lakini sijawahi kuona mafanikio zaidi ya kushinda 100K baada ya kupoteza zaidi ya 200K.

Ni upuuzi tu.
 
Dah,achana na mawazo hayo mkuu.

Mimi nilianza kubet miaka 4 iliyopita lakini sijawahi kuona mafanikio zaidi ya kushinda 100K baada ya kupoteza zaidi ya 200K.

Ni upuuzi tu.
Asante kwa ushauri mdau
 
.
Mkuu ningeshauri usianze kabisa kubet kwa sababu;
.
Ni kinyume na amri ya Mungu katika vitabu vyote vya Wakristo na waislam.
.
Ni mchezo wa Bahati na sibu hivyo huwezi kutengeneza kipato cha uhakika.
.
Ukicheza sana utakuwa addicted, hapo ndio balaa zaidi. Unaweza kufika mahali ukauza kila kitu chako ili tu ukabet kwa matarajio kwamba nitapata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…