nessonlegend
JF-Expert Member
- Mar 1, 2013
- 1,698
- 1,512
Sidhani kama upo kamili mkuu, au STELLES, zimekuandamana.Wamekuomba msaada? Wakati wanazaa hao unaodai wtt waliokimbiwa na na wanaume waliowazalisha hawakujua kama kuna malezi?
mkuuu naomba format ya katiba ya NGOsTARATIBU ZA USAJILI WA NGOs CHINI YA SHERIA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (NGOs) NA. 24 YA MWAKA 2002
Maombi ya usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yatakuwa na viambatanisho vifuatavyo kama ilivyopendekezwa na Sheria hii katika kifungu cha 12(2)
a) Katiba ya Shirika lisilo la Kiserikali
b) Taarifa yenye majina na saini za wanachama waanzilishi
c) Maelezo binafsi ya wanachama na picha
d) Ada ya usajili
e) Anuani na sehemu yalipo makao makuu ya ofisi za Shirika Lisilo la Kiserikali
f) Maelezo yoyote au taarifa kama itakavyohitajiwa na Msajili
Maombi ya usajili wa Shirika Lisilo la Kiserikali yatakuwa kwenye fomu maalum NGO A form No. 1
Maombi ya Cheti cha ukubalifu (certificate of Compliance) yatakuwa na viambatanisho vifuatavyo: -
a) Kivuli halisi cha Katiba ya Shirika Lisilo la Kiserikali.
b) Cheti cha usajili chini ya Sheria nyingine tofauti na Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
c) Taarifa yenye majina na saini za wanachama waanzilishi.
d) Maelezo binafsi ya wanachama na picha
e) Anuani na sehemu yalipo makao makuu ya ofisi za Shirika Lisilo la Kiserikali.
f) Maelezo yoyote au taarifa kama itakavyohitajiwa na Msajili.
Maombi ya Cheti cha ukubalifu yatakuwa kwenye fomu maalum NGO A form No, 3.
ADA
Ada ya usajili ngazi ya Wilaya itakuwa ni Shs 41,500/= kama ifuatavyo:
- Ada ya faili 15,000/ =
- Ada ya usajili 25,000/=
- Stamp duty 1,500/=
Ada ya usajili ngazi ya Mkoa itakuwa ni Shs 56,500/= kama ifuatavyo:
- Ada ya faili 15,000/=
- Ada ya usajili 40,000/=
- Stamp duty 1,500/=
Ada ya usajili ngazi ya Taifa itakuwa ni Shs 66,500/= kama ifuatavyo:
- Ada ya faili 15,000/=
- Ada ya usajili 50,000/=
- Stamp duty 1,500/=
Ada ya Mashirika ya Kimataifa itakuwa ni USD 267 kama ifuatavyo:
- Adayafaili US$ 15
- Ada ya usajili US$ 250
- Stamp duty US$ 2
Kila Shirika lisilo la Kiserikali lililosajiliwa na kupatiwa cheti cha ukubalifu chini ya Sheria hii, linatakiwa kulipa ada ya mwaka ya Shs. 50,000/= au US$ 60 kwa Mashirika ya Kimataifa.
Mashirika haya pia yatapaswa kuwasilisha taarifa zake za kazi za kila mwaka (Annual Report) ambazo zitakuwa kwenye Fomu maalumu NGO A Form Na. 10 kwa Msajili Mkuu kupitia kwa Wasajili Wasaidizi.
Mashirika ya Kitaifa na Kimataifa yatasajiliwa moja kwa moja na Msajili Mkuu. Taratibu zake zitakuwa kama zilivyo taratibu za usajili katika ngazi nyingine isipokuwa kutakuwa na tofauti katika ada ya usajili, halikadhalika maombi ya usajili katika ngazi hizi yatawasilishwa moja kwa moja kwa Msajili Mkuu.
MAMBO MBALIMBALI YA KUZINGATIWA
Utaratibu wa malipo ya ada ya usajili/ mwaka
Malipo ya ada ya usajili wa NGOs na ada za mwaka yatafanyika kama ifuatavyo:
(i) NGOs zote zitakazosajili katika ngazi ya Mikoa na Wilaya watalipa fedha katika Akaunti Nambari 16:29 Miscellaneous Deposit (Akaunti hii ni ya Hazina iliyoko kila mkoa) kwenye matawi ya Benki ya NMB katika maeneo yao.
(ii) NGOs zitakazosajili ngazi ya Kitaifa na Kimataifa watalipa fedha zao katika Akaunti Nambari 16:140 Miscellaneous Deposit (Hazina Ndogo mkoa wa Dar es Salaam). Kiutendaji Idara ya Uhasibu, Ofisi ya Makamu wa Rais itapokea fedha hizo na kutoa stakabadhi halali ya malipo hayo.
KWA MAELEZO ZAIDI NIPM NIKUPE FORMAT YA KATIBA INAYOTAKIWA.
Unaweza kusajiri kupitia wizara ya afya, maendeleo ya jamii, wazee, jinsia na watoto au wizara ya mambo ya ndani.
Hapa Mkuu naona umekuja na mhemko zaidi kuliko kutafuta suluhisho.Wapendwa,
Nimekuwa nikifuatilia issue nyingi za wanawake kwenye jamii wanavyopitia kwenye hali ngumu za kukatisha tamaa, misukosuko kwenye ndoa na hata kwenye malezi ya watoto. Wanake wengi wametelekezwa na wanaume either baada ya kuzaa au baada ya maisha kuwa magumu, wanaume wengi huwakimbia wake zao na kuwaacha na watoto bila kufikiria feature ya hao watoto nabaadae kujirudisha nakudai watoto bila kujali ni msoto gani huyu mama amepitia na hao watoto.
Kwakweli Mimi huwa naumia sana kuona mwanaume ameitelekeza familia au mwanamke naanajua Ana watoto au mtoto, kisaikolojia mama anaumia sana na watoto hapo baadae. Hivi inakuaje mwanaume unajiita mwanaume unatelekeza mtoto, mimba hukubeba wewe, uchungu hukusikia wewe, kero yakulea hukuipata kama mwanamke mtoto unauhakika ni wa kwako, anatumia jina lako halafu kumthamini tuu kwa kumjali hata kidogo umeshindwa?
Nitapigana mpaka nihakikishe imeundwa sheria kali kabisa yakuwaadhibu wanaume wanao watelekeza wanawake na watoto, sheria kali ichukuliwe hakuna sababu yakuendelea kuvumilia hata ustawi wa jamii kwamimi naona bado inawabeba wanaume kuliko kinamama, imagine mwanamke ametelekezwa na mumewe toka mimba, amepitia hali ngumu mateso na kashfa na kudharauliwa juu kama mjuavyo mimba isiyo na baba inavyosimangwa.
Then anajifungua na kulea huyo mtoto mwenyewe kwenye mazingira magumu mno, mtoto anafika miaka sita bila kumjua baba yake, then baba anajitokeza anaanza kudai mwanae tena kibabe hadi ustawi wa jamii anaenda inamaana mkosaji anajipeleka kwenye sheria kudai haki, na ustawi wa jamii wanamuita mama wanadai ampe mtoto baba badala ya baba kushtakiwa au hata kutozwa fine ya maana.
Hivi mnawachukulia wanawake ni watu au wanyama kwakweli wanawake amkeni wakati wakuonewa sio huu, sheria za ustawi wa jamii ziko kimfumo dume na hazitendi haki kabisa, inapaswa mwaume yeyote anayetelekeza watoto, watoto wasiitwe kwa jina lake na uhusiano wana namna yoyote kwenye hiyo familia usiwepo ikiwezekana hata kwakiapo mahakamani, sheria iwe kali watoto wengi hawatendewi haki na kimama wanaonewa.
Sheria za ustawi wa jamii lazima ibadilishwe sheria imekaa kimfumo dume.
Mawasiliano plzTARATIBU ZA USAJILI WA NGOs CHINI YA SHERIA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (NGOs) NA. 24 YA MWAKA 2002