Nataka nifungue biashara ya Mapochi ya kike ya mtumba naomba kujua zinapopatikana

Llio 002

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2015
Posts
1,636
Reaction score
2,053
Habari wana Jf, nina mpenz wangu ambaye hana shughuli yoyote ya kumpatia kipato na kawa tegemezi sana sasa nina taka kumfungulia biashara ya kuuza pochi za kike za mtumba, tatizo sina connection sijuwi wapi nitapata hizo pochi na bei zake huwa wanauzaje mitumbani kwa mwenye uelewa na ufahami juu ya biashara hii naomba anijuze hapo chini waungwana.
Natanguliza shukrani zangu za dhati

Sent using Jamii Forums mobile app
 
zinapatikana katika mabelo ya mtumba na belo yanatofautianabei, mie sijawahi nunua kwahiyo sijui bei exactly, jap tandika nimeona wanao kata na kupiga mnada kwahiyo wanunuzi wananunua then nao wanaenda kuuza na namna wananunua ni kulingana na pochi yenyewe, ikiwa ni mkato mkali na bei inakuwa kali ikiwa mkato wa kawaida bei inakuwa kawaida, kwahiyo watu ambao naweza ita machinga wananunua then nao wanaenda kuziosha zinakaa poa then nao wanauza, wapo wanaotembeza na wapo wanaoweka kwenye vibabda vyao sehemu nyingine na wanakopatia mzigo, ukipata nafasi jaribu pitia kwenye masoko yanayokata belo utapata info zitakazokufaa ila nenda na mlengwa akaone namna biashara inavyofanyika na ajue mikato
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…