Malingumu
JF-Expert Member
- Apr 5, 2012
- 616
- 429
Habari wana JF.
Ni karibu mwaka sasa tangu nimalize masomo yangu ya chuo kikuu na hatimaye kutunukiwa shahada yangu ya kwanza. Nimekuwa nikituma maombi ya kazi sehemu mbali mbali nikiamini kuwa ningefanikiwa lakini mpaka saa hii bado sijafanikiwa kujiajiriwa. Kimsingi napenda kujiajiri ingawaje nilikuwa sina pa kuanzia,sasa hivi majuzi kuna mzalendo mmoja ananipa piki piki kwa mkopo ili niifanyie kazi na hatimaye kurudisha mkopo wote kwa vile tulivyoelewana.
Kilichonisukuma hasa kuja humu ni kujaribu kupata mawazo yenu ya kujua hasa ni "kijiwe" au "route" ipi inafaa na angalau yenye wateja na ambayo haina usumbufu sana wa askari hapa jijini Dar ambayo naweza kupata angalau 20,000 kwa siku maana kwa taarifa zisizo rasmi nilizozipata ni kuwa unaweza kupata hata 30,000-40,000 au zaidi ya hapo kama ukikomaa kwa siku. Nakaribisha mawazo yenu please wadau,nikipata mawazo toka ambaye ame/anafanya kazi hii au hata yule mwenye uelewa /uzoefu katika hili ntashukuru. Naamini piki piki hii itanipigisha hatua na hata baadae kutokuwaza tena kuhusu kuajiriwa.
Karibuni wadau tulijenge taifa.
Asante.