Mkuu umenifungua vya kutosha Ebwana ubarikiwe Sana pia naliskia pale Modern wapo vizuri, Ahsante Sana kwa ushauri mzuri [emoji120]
Yes! Wapo vizuri na Wana magari mengi na ya kisasa kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo ni wewe tu uweke juhudi za ziada kwenye kujifunza na ukiwa na Confidence itakusaidia sana.
Sifa za dereva mzuri:
1) Awe mvumilivu asiwe na hasira anapokuwa barabarani
2) Awe mwepesi kuchukua hatua kila anapoona jambo linaloweza kuleta madhara;
Zingatia haya kila baada ya dakika chache unapoendesha gari...
- Mara kwa mara unapoendesha angalia SIDE MIRROWS kuona kilicho nyuma yako
- Mara kwa mara angalia DASH BOARD yako kupata taarifa za gari lako kupitia sensor na gauge zilizopo kwenye dashboard(Temperature,Oil ,Mafuta,seat belt,Battery.....)
- Mara kwa mara sikiliza SAUTI ya gari yako (engine,body,tairi....) Ili kama kuna kitu hakiko sawa utagundua mapema
- Mara kwa mara sikilizia HARUFU zinazotoka kwenye gari yako kama kuna harufu ya utofauti utagundua mapema( harufu ya Tyre kuungua,plate clutch, Engine kuchemsha, waya kuungua, Mafuta kuvuja....)
3) Asitumie kilevi kupita kiasi anapoendesha gari na azingatie alama na sheria za barabarani.
Nakutakia Kila la heri.