Nataka nimfundishe kijana adabu

MAKULUGA

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2011
Posts
7,828
Reaction score
10,527
Kuna kijana tulimwajiri Saluni kwa miaka kama 2 hivi.

Tulimuamini kupita kiasi ,kuna kipindi alihitaji generator akasema lipo lina uzwa used linafaa ,tukampa laki 4 akanunua .Alitumia GENERATOR HILO MIEZI 2 AKASEMA AMELIPELEKA KWA FUNDI.

bAADA YA MIEZI 3 TUKAMBANA ATUPELEKE KWA FUNDI AKASEMA AMESAFRI ! Baada ya kugundua anatudanganya tukamwambia arejeshe fedha! Wakati hua alishaamua kuacha kazi! Akasema tuandikshane baaday a miezi 2 atalipa ...Hadi sasa ni miezi 5 ! Hajalipa na anaonesha dharau!

Nimetafakari kuwa hawa vijana ni mojawapo ya vijana wengi wajinga wasiojua fadhila .Sasa nimeamua nimshataki leongo kuu ni kumfundisha adabu ....kupitia kwake wengine wajifunze!

Naomba msaada wa kisheria!
 
mbona kesi nyeupe we unataka urudishiwe gharama au unataka akulipe au unaweza endesha vyote ikiisha civil cas ndo ukomo wa kumfungulia kesi ya jinai.
 
Angalia as long as unavyochelewa kumfungulia mashtaka ndivyo muda wa kutomshtaki unavyokaribia (status of limitation).
 
Msamehe tu endelea na maisha yako.
 
Angalia as long as unavyochelewa kumfungulia mashtaka ndivyo muda wa kutomshtaki unavyokaribia (status of limitation).
hiyo ni criminal case haina limitation. alichukua hela kwao akijifanya anaenda kununua generator akazibuya na hakuna generator alilonunua, hapo alijipatia pesa kwa njia ya udanganyifu (obtaining money by false pretence), sijui kesi hii primary court wataifungua kwa kosa gani, siyajui makosa yaliyoko kwenye miongozo ya primary court. ni kesi ndogo mno ambayo haitaenda district au resident maginstrate court ambako wangetumia penal code cap. 16 na kumshitaki kwa kosa hilo la obtaining money by false pretence.

all in all, hiyo hela ni ndogo sana, achilia tu. mpuuze tu. utamsweka ndani dogo kwasababu ya laki nne tu hujui yeye atalose kiasi gani ktika future yake kwa kwenda jela kwa laki nne tu. wakati mwingine tunahitaji kuwa watu wa kuachilia na kusamehe kwasababu hujui yatakayotokea mbele yenu kati yako na huyo kujana. si ajabu ndio huyo utakuja kujikuta umeugua akakuchangia figo wakati watu wote hawajajitokeza au akakuokoa kitu fulani, samehe bure na endelea na maisha yako, laki nne ni hela ndogo sana haifikii thamani ya kumburuza dogo mahakamani na kwenda jela.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…